Divali

Divali ni sikukuu kwenye Uhindu

Divali ni sikukuu ya mwanga au mwangaza. Mwangaza unasaidia miungu kuondoa giza. Yale mazuri lazima yashinde dhidi ya mabaya. Mwangaza na mapambo ya aina ya rangoli kwenye mlango, yanawakaribisha wageni na miungu mema. Roho mbaya inapaswa kuwa mbali.

Hakuna njia ya kudumu jinsi ya kusherekea divali. Kunaweza kuwa na sherehe katika sehemu mbalimbali. Divali inasherekewa mwishoni mwa mwezi wa kumi ama mwanzoni mwa mwezi wa kumi na moja. Kwenye Divali familia hujipamba kwa nguo nzuri. Wengi wanapamba mikonoyao na hina. Ni kawaida kusherekea na familia na marafiki. Wanakula chakula kizuri, keki na pipi. Wengi hupeana zawadi.Wengine pia hupiga fataki.

Wahindu wanaamini kwenye miungu wengi. Lakshmi ni Mungu wa mwanga au mwangaza, kuwa vizuri na utajiri. Wahindu wanatamani Lakshmi awatembelee nyumbani mwao wakati wa divali. Yeye huwaondoa pepo wabaya. Divali inawakumbusha pia kuhusu miungu Rama na Sita kuwa wamekuja nyumbani baada ya miaka mingi wakikimbia.

Wahindu wanaomba Mungu na kutoa sadaka za zawadi chini ya divali. Wanaita puja. Wanaweka chakula, vinywaji, taa na uvumba au ubani.Wengi wanaimba au kucheza. Ni kawaida kusafisha sanamu ya miungu na kupamba na poda yenye rangi. Watu wengi huenda kwenye hekalu (jumba kubwa) na kutembelea marafiki. Wanatakiana divali njema na kutuma kadi za divali.

Lær mer om hinduismen