Jødedommen // Dini ya kiyahudi

Denne teksten finnes på flere språk. Tanken er at teksten skal være et supplement til andre læremidler og andre aktiviteter i opplæringen. Det er altså ikke meningen at disse ressursene skal stå alene, men at de kan brukes i innledning til arbeid med temaet.

Teksten kan, for eksempel, brukes sammen med tospråklig lærer for å aktivere elevenes kunnskaper om temaet, og å bidra til at eleven lærer fagspråk.

Uyahudi au dini ya kiyahudi inakadiriwa ilianzishwa miaka 4000 iliyopita. Neno Myahudi linamaanisha mtu ambaye asili yake ni wa taifa la Kiyahudi , iwe kidini, kitamaduni au kikabila.

Kuna Wayahudi karibia milioni 15 duniani. Wengi wao wanaishi nchini Israeli au Marekani (USA). Dini ya kiyahudi inafanana na dini ya kikristo na kislamu katika Imani ya kuamini Mungu mmoja ni muhimu sana kwa Uyahudi. Uyahudi ndio dini ya zamani zaidi kati ya dini tatu za Mungu mmoja.

Dini ya kiyahudi ipo na mwelekeo au madhehebu mbalimbali yanayo tafsiri na kufanya dini katika njia tofauti. Kuna uyahudi wa kiorthodoksi,Uyahudi wa Kihafidhina (conservative) na Uyahudi wa Mageuzi (reform) , hii ni mifano ya mwelekeo tofauti wa kiyahudi.

Imani 

Wayahudi wanaamini katika Mungu mmoja. Mungu ameumba dunia, na anatoa muongozo kwa watu kupitia sheria zake. Uyahudi ulianza na agano kati ya Mungu na Abrahamu. Mungu alifanya makubaliano maalum na Abrahamu. Mungu aliahidi kwamba Abrahamu atakuwa baba wa taifa kubwa, na kwamba watu wa Abrahamu watapewa nchi ya Kanani. Kwa upande mwingine, Abrahamu na kizazi chake walipaswa kumfuata Mungu na kuishi kulingana na sheria zake.  

Katika Uyahudi, mambo muhimu ni upendo, msamaha na haki. Imani inaongoza maisha ya kila siku. Kuna sheria za ndani na desturi kuhusu chakula, mavazi (nguo), sala na sikukuu. Wayahudi wanafuata sheria hizi, ili kudumisha uhusiano wa karibu na Mungu. 

En mann og en gutt kledd i jødisk ortodokse klær
Watu wa dhehebu la dini ya Ortodoski Katika mahujaji (sala) wakati wa ibada katika sinagogi.

Watu watakatifu

Katika Uyahudi, mababu Ibrahimu na watoto zake wa kiume, Isaka na Yakobo, wanachukuliwa kuwa watu watakatifu. Wanaonekana kama mababu wa watu wa Kiyahudi na ndio kiini cha agano na Mungu.

Musa anachukuliwa kuwa nabii aliye kuwa mkubwa zaidi. Yeye alipata amri kumi za Mungu katika mlima Sinai. Aliwasaidia kuwatoa utumwani Wayahudi kutoka nchini Misri.

Uyahudi au dini ya kiyahudi haina watakatifu, ila ina watu wengi walio watakatifu. Hawa ni watu wa mfano wa kuigwa katika imani, uongozi na utiifu dhidi ya Mungu.

Moses går foran mange mennesker
Musa anawasaidia Wayahudi kutoka utumwani Misri.

Vitabu takatifu

Tanakh ni kitabu kitakatifu ambacho kinaunda msingi wa imani na utamaduni wa Kiyahudi. Tanakh ni mwongozo wa kihistoria na wa kiroho, unaowasilisha sheria za Mungu na historia ya Israeli. Tanakh ina sehemu tatu. Sehemu muhimu zaidi ni Torati. Torati ina vitabu vitano vya Musa vyenye sheria, miongozo ya kimaadili na hadithi za zamani. 

Talmud ni maandiko yanayotafsiri Tanakh. Talmud inaelezea jinsi gani mtu anatakiwa aishi maisha ya kidini na kuelezea sheria za wayahudi na majukumu ya vitu wanavyopaswa kuvifanya. Wale wanaotafsiri Tanakh ni wataalamu wa sheria wanaitwa marabi (rabbinere).

Toraen, svart med bilde av menorah på bokomslaget
Torati yenye picha ya menorah

Nyumba ya Mungu (Sinagogi)

Nyumba ya Mungu katika dini ya Wayahudi inaitwa sinagogi. Sinagogi ni sehemu muhimu ya kukusanyika pamoja kidini kwa ajili ya shughuli za pamoja kijamii. Wayahudi hukutana huko kwa ajili ya sala, kujifunza na ibada ya pamoja ya kumuomba Mungu. Sinagogi pia hutumika kwa kufundisha, kusherehekea sikukuu na shughuli zingine zinazojenga umoja.

Sehemu muhimu katika Sinagogi ni aron ha-kodesh, inayomaanisha kabati takatifu. Ndani ya kabati wanahifadhi Torati iliyowekwa kwa kuzungushwa. Sinagogi zinaweza kuwa kubwa au ndogo, na zinaweza kutengenezwa kwa njia tofauti, lakini siku zote huwa zimeelekezwa upande wa Yerusalemu.

Sikukuu na ibada au sala za matambiko

Uyahudi una sikukuu na Sala za matambiko au mila nyingi zinazoashiria matukio muhimu katika historia ya dini na katika maisha ya Wayahudi. Miongoni mwa sikukuu muhimu zaidi ni Sabato, Pesach, Yom Kippur na Hanukkah.

Sabato inasheherekewa kila juma au wiki, kutoka jua linapochomoza siku ya ijumaa (siku ya tano) hadi jua linapozama jioni (magharibi) siku ya jumamosi (siku ya sita). Sabato ni siku ya kupumzika, kusali na kuwa pamoja. Pesaki (pasaka) inasherekewa kuwakumbusha Wayahudi safari ya kutoka Misri na kuwa huru kutoka utumwani.

Yom Kippur inaitwa siku ya upatanisho(kusameheana). Hii ndiyo siku takatifu zaidi ya mwaka, inayotumiwa kwa kutafakari, toba, na kufunga. Hanukkah ni sikukuu ya taa inayosherekewa kwa kuwashwa mishumaa kwenye kinara (stendi ya mishumaa) inayoitwa menorah.

En syv-armet menorah står plassert på et bord, med lysene tent i varme, gylne flammer.
Menorah

Jifunze zaidi kuhusu dini ya kiyahudi