Vesak // Vesaki
Vesaki ni sikukuu kwenye uhindu inayosherekewa siku ambayo mwezi unaonekana wote kwa umbo lake la duara mwezi wa nne au wa tano (mei). Kwenye vesaki wanakumbuka wabudha wote juu ya maisha ya budha. Kwenye vesaki inasherekewa siku ya kuzaliwa budha, hali ya kujitambua na kujua vitu na kufa kwake.
Budha alizaliwa miaka 2500 iliyopita. Jina lake lilikuwa Siddhartha Gautama na yeye alikuwa mtoto wa kiume wa mfalme. Japo kuwa yeye alikuwa na kila kitu alichohitaji, hakuwa na furaha kwa sababu aliona watu wengi wanaomzunguka hawapo vizuri. Wengi walikuwa wagonjwa, wazee, wenye huzuni au wanalio kufa (maiti). Hivyo aliamua kuachana na maisha yake mazuri kama mtoto wa kifalme na kwenda kutafuta jinsi gani watu wanaweza kuwa na maisha mazuri. Alitumia takribani miaka sita kujifunza, kufikiria na kutafakari katika hali ya utulivu.
Mwisho, huku akiwa amekaa chini ya mti mkubwa, alipata majibu aliyokuwa anayatafuta. Alielewa ni jinsi gani mtu anaweza kuishi maisha mazuri na kuwa vizuri. Ndipo alipojulikana kama Budha, inayo maanisha “yule aliyeelimika” . Kuwa mtu aliyeelimika ina maanisha unaelewa vitu kwa uwazi na vizuri. Wabudha wanaita hiyo kujitambua kwa wabudha. Kutoka katika mtoto wa kifalme hadi kuwa Budha.
Budha alitumia maisha yake yote kuwafundisha wengine kile alichokigundua. Aliwafundisha watu kwa nini ni muhimu kuwa wenye roho nzuri na wakweli maishani. Baada ya kifo cha Budha, mafundisho yake yaliendelea kuishi. Haya ndio mafundisho tunayoyajua leo kama Ubudha.
Wakati wabudha wanasherekea Vesaki wanakwenda kwenye hekalu kusikiliza mafundisho ya watawa wanayoyaelezea kuhusu maisha ya Budha. Hekalu linapambwa na maua na kuwashwa mishumaa na kuchomwa ubani au uvumba. Maua yote yanakumbusha kuwa Budha alizaliwa kwenye bustani. Maua ya lotus ni muhimu kwa wabudha. Pale Budha alipotembea hatua zake saba za kwanza kwenye bustani, yaliota na kukua maua ya lotus kwenye alama za nyayo zilizowekwa na miguu yake katika sehemu alizopita. Hekaluni, Wabudha wanainama mbele ya madhabahu za sanamu za wabudha kwa heshima kwa Budha, Dharma na Sanga (watawa wa kiume na watawa wa kike). Wabudha wengi huenda hekaluni ili kuwapa watawa wa kiume chakula. Wengine hutafakari kwa utulivu, kutoa pesa au vitu kwa mahekalu na kwa wale wanaohitaji. Pia ni kawaida na desturi kutoa sadaka ya maji, mchele na matunda mbele ya sanamu mbalimbali za Buddha.
Ni kawaida kwa nyumba, nyumbani na mahekalu kupambwa kwa taa na bendera za Wabudha. Sehemu nyingine wanazituma pia taa na kuziachilia ziende juu angani. Watu wengi hutuma kadi za Vesak ikiwa ni kuwatakia sherehe njema.
Filamu kuhusu Vesaki ya Korea
Jifunze zaidi kuhusu uhindu
Alle bilder er hentet fra Adobe Stock