Den kristne påskefortellingen // Sikukuu ya pasaka ya Kikristu
Yesu alipokuwa mtu mzima, alisafiri pamoja na wanafunzi wake 12, watu wote waliokutananao waliwaeleza kuhusu Mungu. Yesu alikuwa mtu mwema na mkarimu aliyesaidia watu masikini kiimani na kuponya wagonjwa.
Yesu alipata marafiki na maadui wengi. Baadhi ya viongozi hawakupendezwa jinsi umati wa watu au kundi kubwa la watu lilivyokuwa linasikiliza mafundisho ya Yesu na kumfuata yeye kuliko wao. Walikuwa wanaogopa kuwa Yesu atakuja kuwa na nguvu kubwa.
Jumapili ya matawi

Jumapili moja kabla ya pasaka Yesu na wanafunzi wake walisafiri mpaka Yerusalemu, kwajili ya kwenda kusherekea sikukuu ya pasaka.
Aliwaomba wanafunzi wake wawili watafute punda. Yesu alipanda juu ya punda na kuelekea Yerusalemu. Alisalimiwa kama mfalme na watu aliokutana nao njiani. Walisema “Hossiana! hossiana, mfalme wetu amekuja!” Walimpungia kwa matawi ya mtende makubwa kama bendera. Hosianna ina maana sawa kama hurra (kwa lugha ya Kinorway).
Alhamisi kuu – Ushirika wa Kikristu

Jioni Yesu alikula chakula cha pasaka pamoja na wanafunzi wake. Kipindi hicho ilikuwa kawaida kuosha miguu kabla hawajaingia ndani, kwa sababu walitembea bila viatu ama walivaa viatu vya wazi, na kuchafuka miguu. Katika Mlango wa nyumba, Yesu aliwaosha miguu wanafunzi wake. Alifanya hivyo kuonesha kuwa wote wanapaswa kusaidiana.

Walipokuwa wamekaa na kula, Yesu alisema: “Sasa si muda mrefu nitakamatwa na kufungwa, na kisha nitakufa”. Pia alisema mmoja wa wanafunzi wake atawasaidia askari kumkamata.

Yuda mwanafunzi wa Yesu, aliamini kuwa Yesu atakuja kuwa tajiri na mfalme mwenye nguvu. Alipoona Yesu hajali kuhusu pesa na nguvu, alimkasirikia Yesu.
Baada ya chakula ilikuwa ni muda wa jioni. Yesu alienda pamoja na wanafunzi wake mpaka kwenye bustani. Hapo Yesu alifanya ibada kwa Mungu. Yuda aliwaongoza askari mpaka kwenye bustani na kuwaonesha mahali Yesu alipokuwa. Kwa kufanya hivyo Yuda alipatiwa vipande 30 vya fedha. Yesu alijua Yuda atakuja kufanya hivyo, hivyo kwa hiyari yake (kwa kuamua mwenyewe) aliwafuata askari waliokuja kumkamata.
Ijumaa kuu – kuhojiwa, hukumu, kusulubiwa na kuzikwa
Yesu alijua kuwa atakufa. Mungu alipanga hivyo kwa muda mrefu. Tangu Yesu alipokuja duniani alijua hilo litatokea. Alizaliwa kuchukua adhabu ya makosa yote ya binadamu waliyofanya na watakayo kuja kufanya. Muda ulikuwa umewadia, askari walimpeleka kwa viongozi wao. Hawakuamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu. Walisema: “Anapaswa kufa kwa sababu anajiita mwana wa Mungu”. Walimtundika Yesu msalabani katika sehemu iitwayo Golgota. Hapo Yesu alikufa.

Kwa takribani miaka 2000 iliyopita hii ilikuwa njia ya kawaida ya kuwaadhibu wahalifu. Ilikuwa siku ya kusikitisha kwa wanafunzi na marafiki wa Yesu. Hawakujua Mungu amepanga maajabu ya kushangaza makubwa kwao. Wasingeendelea kuwa na huzuni kwa muda mrefu sana.
Mkesha wa pasaka– sehemu ya kaburi inalindwa

Baada ya Yesu kufa , marafiki zake walimuweka ndani ya pango. Pango walilipata toka kwa mtu mmoja aitwaye Yosefu.
Yosefu alitaka mwana wa Mungu apate hii zawadi ya mwisho toka kwake. Walilifunga pango kwa jiwe kubwa katika sehemu ya kuingilia. Kiongozi alituma askari wawili kulinda eneo hilo ili asije tokea mtu yoyote kuiba mwili wake Yesu.
Siku ya kwanza ya pasaka
Mapema asubuhi ya jumapili lilitokea tetemeko kubwa la ardhi. Malaika toka mbinguni alishuka na kusukuma jiwe lile kubwa, lililokuwepo kwenye mlango wa kuingia kwenye pango alipozikwa Yesu. Walinzi walipomuona malaika walitetemeka kwa hofu na kukimbia.
Baadae kidogo walikuja moja kati ya marafiki wa Yesu, Maria na Maria Magdalena. Walipoona jiwe halipo mlangoni waliingia ndani ya pango na kumuona malaika. Malaika alisema: Mnayemtafuta“Yesu” hayupo hapa, amefufuka, nenda kawaambie marafiki zake wote watamuona tena!”
Maria na maria Magdalena hakuwa na huzuni tena. Yesu hakuwa amekufa. Alikuwa hai. walikimbia na kurudi kuwaeleza watu habari njema.

Siku ya pili ya pasaka
Mara ya kwanza hakuna mwanafunzi wa Yesu alieamini kile Maria na Maria Magdalena walichosema. Lakini Maria alikuwa akisema kweli. Siku ya pili ya pasaka Yesu anakuja kukutana nao tena. Ni kweli amefufuka toka kwa wafu.
Kupaa kwa Yesu mbinguni
Baada ya siku 40 Yesu aliwachukua wanafunzi wake mpaka kwenye sehemu iliyokuwepo karibu na mlima mkubwa. Yesu alinyoosha mikono yake juu na kuwabariki. “Waelezeni watu wote juu yangu mimi”, alisema. Kisha akapaa juu mbinguni.
Siku hiyo inaitwa kupaa kwa Yesu (kwa lugha ya Norway Kristi himmelfartsdag). Wingu lilimfunika na hawakumuona tena. Walisimama wakitazama mawinguni / angani kwa muda mrefu.
Ghafla walitokea malaika wawili kati kati yao. “Kwanini bado mmesimama mkiangalia mawinguni / angani?” waliuliza “Yesu amepaa mawinguni. Siku moja atarudi tena kwa njia ile ile kama vile mlivyo muona akienda mbinguni.”
Hivyo wanafunzi wake walirudi mjini wakiwa na furaha moyoni. Yesu alikuwa amewa fundisha mambo mengi sana. Siku zote watakumbuka alisema: “msiwe na hofu wala uoga. Muaminini Mungu na mimi. Ndani ya nyumba ya Mungu kuna vyumba vingi. Mimi ninakwenda kuwaandalia makao kwa ajili yenu. Siku moja nitarudi tena na kuja kuwachukua ili mahali nilipo mimi na nyinyi muwepo”.

Illustrajoner fra Adobe Stock