Hinduismen // Uhindu
Uhindu ni moja ya dini zenye miaka mingi duniani. Mtu anaeamini kwenye uhindu anaitwa mhindu. Uhindu ni dini ya tatu kwa ukubwa duniani.
Imani
Wahindu wanaamini vitu vyote katika ulimwengu vimeunganishwa na kuongozwa na sheria zilizoamuliwa. Binadamu, wanyama na mimea wapo na kazi maalumu, hii inaitwa dharma.
Wahindu wanaamini vyote vinavyozaliwa, vinakufa na kuzaliwa upya au tena. Hii inaitwa kuzaliwa tena au upya. Na hii inaelezewa kama samsara. Kama utaishi maisha mazuri, unaweza kuepuka kuzaliwa upya. Kisha utakuwa umewekwa huru kutoka maisha ya duniani, na unaweza kuishi pamoja na miungu. Hii inajulikana kama moksha.
Miungu
Katika uhindu kuna mamilioni ya miungu, tamaduni na historia tofauti. Baadhi ya miungu ni muhimu mfano; Mungu Brahma, Vishnu na Shiva. Brahma ni Mungu alieumba dunia na anaongoza vyote alivyoumba. Vishnu ni Mungu anaeangalia dunia na kuchunga kile kitakacho mtokea binadamu. Mungu Shiva anaharibu kila kitu, lakini yeye ni yule anaeumba tena maisha mapya. Ingawa kuna miungu mingi, Mhindu angesema kwamba miungu yote ni toleo la nafsi ya Brahman. Kuna nguvu iliyopo ndani ya vitu vyote vinavyoishi.
Hekalu la kihindu
Mahekalu ni nyumba za kiroho za wahindu. Jinsi mahekalu yanajengwa na kupambwa ni tofauti katika sehemu mbalimbali duniani, lakini picha ya miungu na sanamu ni kitu cha kawaida sehemu zote. Kila hekalu la kihundi limejengwa kwa heshima ya mmoja wa miungu, lakini linaweza kuwa na sanamu au picha za miungu wengi.
Maandiko matakatifu
Kuna maandiko mengi matakatifu katika uhindu. Yanaelezea nini ni sawa na nini si sawa kufanya katika maisha na jinsi gani wahindu wanapaswa kufuata dini yao. Maandiko mengi yana miaka zaidi ya maelfu toka yaandikwe. Wahindu wengi wanasikiliza maandiko matakatifu wakitembelea hekalu. Anaesoma maandiko anaitwa brahmin. Brahmin ni mchungaji.
Puja
Puja maana yake ni kumuomba mungu. Wahindu wanaweza kuabudu miungu wakiwa katika hekalu, katika nyumba zao kwenye madhabahu au sehemu ya nje katika uwanja wenye hewa na wazi. Puja inafanyika mbele ya sanamu ama picha ya miungu. Wahindu wanasafisha sanamu za miungu na kuweka maua, chakula na maziwa. Mtu anawasha mshumaa, anachoma uvumba au ubani, anaimba na kuomba.
Maisha ya kila siku
Kufikiria juu ya vitu vyote vinavyoishi kwenye uhindu ni kitu muhimu sana. Ndio maana kuna sheria muhimu sana kwamba mtu hapaswi kuumiza kitu kinachoishi. Ngómbe wanaonekana kama watakatifu. Ngómbe wanatoa maziwa ambayo binadamu anahitaji. Binadamu wanakunywa maziwa toka kwa mama tunapokuwa watoto, lakini tunakunywa maziwa ya ngómbe maisha yetu yote. Wahindu wanaona ngómbe kama mama kwa watu wote. Ngómbe ana kazi nyingi muhimu za kufanya, ndio maana watu wengi kwenye dini ya uhindu wamejenga ukaribu sana na ngómbe. Ndio sababu hawali nyama ya ngómbe.
Uhindu ni moja ya njia ya jinsi ya kuishi. Ni kile nini mtu anafanya na si kile mtu anachoamini, ndio kinachoamua. Kuonesha heshima au nidhamu ni muhimu, kwa mfano ni muhimu kuonesha heshima au nidhamu kwa watu wakubwa au wazee. Pale watoto wanapokutana na wazee au watu wakubwa katika familia wanaonesha heshima, kwa kushikanao mkono na kusalimia nao. Na watoto wanapewa baraka toka kwa watu wakubwa wanaowasalimia.
Sikukuu za kihindu na ibada za matambiko
Wahindu wapo na sikukuu nyingi tofauti. Ni ngumu kuweza kuhesabu na kujua kuna sikukuu ngapi zinazopatikana. Kuna sikukuu ndogo zinazosherekewa tofauti katika sehemu tofauti na sikukuu kubwa zinazosherekewa kote katika dunia ya wahindu. Sikukuu inaweza kuwa juu ya matukio yanayoelezea asili ya watu (mytholojia) na juu ya matukio ya kila siku au vyote viwili kwa pamoja. Divali na Holi ni sikukuu mbili katika Uhindu. Divali ni sikukuu ya mwanga au mwangaza. Mwangaza unasaidia miungu kufukuza giza na kwamba yale mazuri yatashinda dhidi ya mabaya. Holi ni sikukuu ya rangi. Holi inasherekewa mwanzoni mwa msimu wa mvua na rangi zote zinatakiwa kuashiria kutamani mwaka mpya wenye aina mbalimbali ya mimea yenye utajiri wa rangi.
Ibada au tambiko la mpito au la kuvuka hatua ni muhimu katika uhindu. Sherehe ama matukio mbalimbali wanasherekea wahindu kuvuka toka hatua moja ya maisha mpaka nyingine kwa mfano ndoa ama kutoka utoto kwenda kwenye ujana. Sherehe nyingine ni ibada ya kamba takatifu (snor-ritualet). Katika ibada hii, watoto wa kiume hupewa kamba nyekundu karibu na mkono wao. Wanakaribishwa katika dini na sasa wako tayari kujifunza maandiko matakatifu. Sikukuu na ibada huadhimishwa kwa utofauti katika nchi mbalimbali na maeneo tofauti na kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu mwingine.
Maeneo matakatifu kwa wahindu
Nchini India wanaishi wahindu wengi. Ndio maana maeneo mengi nchini India ni matakatifu kwa wahindu. Wahindu huamini kwamba kuwa katika mahali patakatifu huleta wokovu. Mto Ganges na maeneno ya milima ya Himalaya inachukuliwa kuwa ya kimungu. Wahindu wanaamini kwamba Mungu Shiva ameunganishwa na milima ya Himalaya na mto Ganges. Kuoga katika Ganges ni kitendo cha kiibada. Inayosafisha na kuokoa. Watu wengi husafiri hadi Ganges na katika mji mtakatifu Varanasi kama watu wanaofanya safari ya kidini sehemu takatifu (kuhiji au kwenye mahujaji) kwa kufanya matambiko.
Jifunze zaidi kuhusu uhindu
Bildekort: Divali
Bildekort med ord, bilde og lyd som handler om høytiden Divali
Høytidskalender: Divali (ekstern lenke)
Les om Divali. Veilederkorpset i Stavanger kommune har publisert en flerkulturell kalender som viser ulike høytider.
Høytidskalender: Holi (ekstern lenke)
Les om Holi. Veilederkorpset i Stavanger kommune har publisert en flerkulturell kalender som viser ulike høytider.