FN – en møteplass for fred // Umoja wa mataifa – sehemu ya mkutano kwa ajili ya amani

Denne teksten finnes på flere språk. Tanken er at teksten skal være et supplement til andre læremidler og andre aktiviteter i opplæringen. Det er altså ikke meningen at disse ressursene skal stå alene, men at de kan brukes i innledning til arbeid med temaet.

Teksten kan, for eksempel, brukes sammen med tospråklig lærer for å aktivere elevenes kunnskaper om temaet, og å bidra til at eleven lærer fagspråk.

Umoja wa mataifa ulianzishwa mwaka 1945, baada ya kumalizika vita kuu ya pili ya dunia. Matumaini yalikuwa kwamba shirika la kimataifa linaweza kuwa chombo kitakachozuia vita kutokea siku za mbeleni na kufanya kazi kwa ajili ya kutunza amani. Nchi 51 zilikubaliana na kusaini mkataba unaoitwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Mkataba huu ulianza rasmi tarehe 24-10-1945, ndiyo maana siku ya Umoja wa Mataifa huadhimishwa tarehe hiyo kila mwaka. Leo, karibu nchi zote duniani ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Katibu mkuu

Umoja wa mataifa unaongozwa na katibu mkuu. Katibu mkuu huchaguliwa na baraza kuu na anaongoza kwa kipindi cha miaka mitano. Kazi yake ni kuongoza kazi za kila siku za Umoja wa mataifa. Kazi nyingine muhimu ni kufanya kazi ya kisiasa kuzuia migogoro isianze, isiendelee au isisambae. Katibu mkuu pia anapeleka matatizo ambayo yanaweza kutishia amani duniani katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Kazi ya umoja wa mataifa

Umoja wa mataifa ni shirika lenye idara au ofisi zenye kufanyia kazi mambo mbalimbali ambayo umoja wa mataifa wanayafanyia kazi. Kazi za umoja wa mataifa zinaweza kugawanya katika maeneo makuu matatu amani na usalama, haki za binadamu na maendeleo endelevu.

Amani na usalama

Baraza la usalama la umoja wa mataifa ndio lina fanya kazi ya kuhakikisha kuna amani na usalama. Kazi kuu ya baraza la usalama la umoja wa mataifa ni kudumisha amani na usalama duniani. Ikiwa amani itakuwa hatarini, Baraza la Usalama kwa kawaida huhimiza pande husika kutafuta suluhisho la amani kwa kuchukua hatua kama vile kuanzisha mazungumzo ya upatanishi. Baraza la Usalama pia linaweza kulazimisha maamuzi kutekelezwa kwa kuamuru vikwazo vya kiuchumi au kuchukua hatua za kijeshi. Mfano wa hatua ya kijeshi ni vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa. Vikosi hivi vinajumuisha wanajeshi walioazimwa/waliokopwa kutoka nchi mbalimbali wanachama.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lina wawakilishi 15 toka nchi wanachama 15. Nchi 5 ni wanachama wa kudumu, nchi nyingine zinachaguliwa kila baada ya miaka 2. Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na China ni nchi wanachama wa kudumu. Katika umoja wa mataifa ni baraza la usalama pekee linaloweza kutumia nguvu za kijeshi na nchi wanachama wote wanajukumu la kufuata maamuzi ya baraza la usalama.

Haki za binadamu

Eneo lingine muhimu la Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha kwamba watu wote wanapata haki za msingi. Tangu mwaka 1948, Umoja wa Mataifa ulikubaliana juu ya “Tamko la Dunia kuhusu Haki za Binadamu”, linaloitwa pia Tamko la Haki za Binadamu. Nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekubali kuhakikisha kuwa haki hizi za binadamu zinalindwa.

Umoja wa mataifa unafuatailia hali ya haki za binadamu duniani na kuhakikisha wanachama wanakutana kwa ajili ya kuendelea kulinda na kuimarisha haki za binadamu.

Maendeleo endelevu

Eneo la tatu muhimu ni maendeleo endelevu. Kazi hii imeelezwa katika Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa. Kuna malengo 17, kama vile kusimamisha mabadiliko ya tabianchi, kumaliza umaskini na njaa, na kuhakikisha usawa wa kijinsia na elimu bora. Lengo ni kufanikisha malengo haya kabla ya mwaka 2030.

Mkutano mkuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hukutana kila mwaka kwa vikao. Kikao kimoja kawaida huanza mwezi wa tisa /Septemba hadi mwezi wa kumi na mbili/Desemba. Baraza Kuu lina wawakilishi kutoka nchi zote wanachama, na kazi yake kuu ni kutoa mapendekezo kwa nchi hizo kuhusu masuala ya ushirikiano wa kimataifa, amani na usalama, maendeleo na haki za binadamu. Mapendekezo haya huitwa maazimio. Azimio la Umoja wa Mataifa ni muhimu sana. Ingawa ni pendekezo tu kwa nchi wanachama, linaonyesha maoni ya jumuiya ya kimataifa. Ili azimio likubaliwe na Baraza Kuu, linahitaji kupata kura sehemu mbili ya tatu au theluthi mbili ya kura zote. Kila nchi mwanachama ina kura moja, na kura zote zina uzito sawa.

Baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa unajumuisha mashirika, mifuko na mipango mbalimbali inayotekeleza kazi za Umoja wa Mataifa. Baadhi ya mashirika ni:

Unicef sin logo. Et lyseblått kvadrat de det står UNICEF  for hvert barn med hvit skrift.. En tegning av jordkloden , symbol av en voksen som holder er barn.

UNICEF – Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto. Wanafanya kazi ya kuwasaidia watoto kote duniani. Dokumenti inayoongoza UNICEF inaitwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto. Mkataba huu unasema kuwa watoto wana haki ya kulindwa kwa namna ya kipekee.

hvit tegning på lyseblå bakgrunn. Tegningen viser et bygg der bokstavebe UNESCO symoliserer søyler

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, Utamaduni na Mawasiliano (UNESCO). Kwa kushirikiana katika maeneo UNESCO inahusika nayo, inachangia kulinda amani na usalama. UNESCO wanataka kuwafahamisha, kuhamasisha na kuwashirikisha watu ili kukuza uelewa na heshima kwa kila mtu na kwa sayari/dunia yetu.

lysebl bakgrunn. hvit ekst der ser står World Health Organisation. Tegning av jordkloden med en slange som vikler seg rundt en pinne

WHO – Shirika la Afya Duniani (WHO). Wanafanya kazi kuhakikisha kila mtu apate afya bora iwezekanavyo. Kazi ya WHO ni kufuatilia, kuchunguza na kuwapatia watu taarifa za kuaminika kuhusu afya na magonjwa. Kwa mfano, WHO huhamasisha na kusaidia kutengenezwe chanjo za magonjwa hatari.

OHCHR – Kamisheni ya Juu ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu. Wana jukumu la kukuza na kulinda haki na uhuru wa kila mtu kama ilivyoelezwa katika Tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu.

Hii ilikuwa ni baadhi ya mifano ya kazi inayofanya Umoja wa Mataifa. Watu wengi duniani wanakubaliana kuwa Umoja wa Mataifa ni sehemu muhimu ya kukutana, ambapo wanachama wote wanazungumza pamoja na kukubaliana kuhusu sheria zipi zitatumika katika siasa za kimataifa.

Kazi ya kufanya kuhusu maneno kutoka kwenye andiko

*

Arbeidsoppgaven inneholder sentrale ord i den norske teksten.

  • Oversett ordene ved hjelp av LEXIN.
  • I høyre kolonne er ordet brukt i en setning som finnes i teksten. Oversett eller forklar hva setningen betyr.

Viktige ord i “FN-en møteplass for fred”

Viktige ord i “FN – en møteplass for fred”

Chanzo

  • Fn-sambandet, https://fn.no/
  • NDLA, FN – en verdensorganisasjon for fred – Samfunnskunnskap – NDLA

Jifunze zaidi kuhusu Umoja wa Mataifa