FNs bærekraftsmål // Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa mataifa

Ressursen er utviklet i samarbeid med FN-sambandet.


Tokomeza umaskini

ikoner av personer i alle aldre

Watu wengi sana wanaishi katika umasikini uliozidi sana/kithiri. Ili kupambana na umaskini, watu wote lazima wapate nafasi/fursa sawa za shule, kazi na huduma za afya. Kwa kuongezea, lazima kuwe na tofauti ndogo kati ya maskini na tajiri. Lazima tugawanye fedha vizuri ndani ya nchi na kati ya nchi na nchi.


Mtu yeyote asiwe na njaa

Illustrasjon av en suppebolle med varmt innhold

Watu wengi huathiriwa na njaa, na kila mwaka kuna watu wengi zaidi na zaidi wanaoathirika (kupata shida) na njaa. Nusu ya watoto wote wanaokufa, hufa kwa sababu wamekula chakula kisichofaa au wamekula chakula kidogo. Kwa hiyo ni lazima tuhakikishe watu wote wanapata chakula wanachohitaji.


Afya bora kwa wote

Illustrasjon av en livslinje med et hjertet

Duniani kote, afya za watu zinaboreka kila wakati. Watu wengi zaidi wanapata chanjo, na watu wanaishi muda mrefu zaidi kuliko hapo awali. Ili kufikia lengo la afya bora kwa wote, ni lazima watu wote wapate huduma za afya na dawa wanazohitaji.


Kila mtu lazima afundishwe vizuri shuleni

Illustrasjon av en bok og en blyant

Kwa bahati nzuri, watoto wengi zaidi wanakwenda shule leo kuliko zamani. Hata hivyo, bado kuna watoto wengi sana ambao hawajui kusoma na kuandika. Kwa hivyo, nchi zote duniani lazima ziendelee kufanya kazi ya kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata nafasi/fursa sawa ya elimu bora na bure.


Wasichana na wavulana lazima wawe na nafasi / fursa sawa ya maisha mazuri

Illustrasjon en tegnet for kjnønn med erlikhetstegn i midten

Haki za binadamu za Umoja wa Mataifa zinatumika kwa watu wote. Hata hivyo, kuna wanawake wengi zaidi duniani ambao ni maskini kuliko wanaume. Pia kuna wavulana wengi zaidi ambao wanaruhusiwa kwenda shule kuliko wasichana. Ili kufikia lengo la usawa, wasichana na wavulana lazima wapate elimu, huduma za afya na kazi zenye malipo/mshahara.


Kila mtu lazima awe na maji safi na choo salama

Illustrasjon ev vannbeger som tømmes

Kuna maji safi ya kutosha kwenye sayari, lakini sio kila mtu anayeweza kupata maji safi ya kunywa. Kila mwaka, mamilioni ya watu hufa kutokana na magonjwa wanayopata kwa sababu hawana maji safi na vyoo. Kwa hiyo, ni lazima tujenge mifumo ya maji safi na maji taka/machafu pale inapokosekana.


Kila mtu anapaswa kuwa na uwezo wa kutumia umeme ambao hauharibu hewa na ardhi

Illustrasjon av en sol med en på- knapp i midten

Sisi binadamu tunahitaji nishati/nguvu kwa ajili ya mwanga/taa, joto na kupikia. Leo sehemu kubwa ya watu hutumia nishati chafu kwa kupikia, na wanakabiliwa na uchafuzi wa hewa. Maji, upepo na jua ni vyanzo vya nishati/nguvu visivyoisha na vinaweza kuchangia katika kufikia lengo la maendeleo endelevu.


Kila mtu anapaswa kuwa na kazi iliyo salama na apate kipato cha kutosha

Illustrasjon av en graf som går oppover

Watu wengi hufanya kazi mahali pa kazi ambapo hapazingatii usalama na haki za wafanyakazi. Watoto wanakabiliwa na ajira za watoto au kazi za kulazimishwa. Ili kuondoa umaskini na kupambana na ukosefu wa usawa duniani, kila mtu lazima awe na kazi salama na yenye kuzingatia haki.


Inatupasa kuvumbua vitu vipya na kutengeneza mifumo mizuri

Illustrasjon av 4 kuber som stables

Ili jamii ifanye kazi, ni muhimu kuwa na mifumo mizuri ya trafiki (vyombo vya usafiri barabarani, angani au kwenye maji), viwanja vya ndege, reli, mabomba ya maji, maji taka, vifaa vya kutupa takataka, nishati/nguvu na mtandao wa intaneti. Ili kufikia lengo hili, lazima tuone jinsi nchi zote zinavyoweza kutumia vyema rasilimali zao na viwanda vyao.


Lazima kuwe na utofauti mdogo kati ya maskini na tajiri

Ikon. FNs bærekraftsmål nummer 10. Tegning av en firkant med et er-lik-tegn inni.. Tekst: Mindre ulikhet

Leo, kuna tofauti kubwa kati ya matajiri na maskini kuliko hapo awali. Kuna tofauti kubwa ndani ya nchi na kati ya nchi na nchi. Ili kufikia lengo la kuwa na tofauti ndogo, kila mtu lazima awe na ufikiaji sawa wa shule na huduma za afya. Pia, rasilimali (vitu muhimu na vya thamani) lazima zigawanywe kwa haki zaidi.


Miji duniani inapaswa kutunza watu na ardhi

Ikon. FNs bærekraftsmål nummer 11. fire forskjellige hus eller bygninger. Tekst: Byer og lokalsamfunn

Zaidi ya nusu ya watu duniani wanaishi mijini. Miji mingi inakua haraka sana kiasi kwamba hakuna kazi na nyumba za kutosha kwa kila mtu. Lazima tujenge miji endelevu inayozingatia mahitaji ya watu, na sio kuathiri hali ya hewa.


Tusitengeneze na kutumia zaidi ya kile tunachohitaji

Ikon. FNs bærekraftsmål nummer 12. Tegning av en pil som er formet som tegnet for uendelig. Tekst: Ansvarlig forbruk og produksjon

Leo tunatumia zaidi kuliko vile sayari (dunia) inaweza kuhimili/kuvumilia. Tunatupa moja ya tatu ya sehemu ya chakula kilichotengenezwa. Ili tuweze kuishi vizuri leo na katika siku zijazo, lazima tubadili mtindo wetu wa maisha na kutumia vitu kidogo. Ni muhimu kwa watu binafsi na makampuni kutumia vitu kidogo na kutunza hali ya hewa.


Nchi zote lazima zifanye kazi pamoja kusimamisha /kukomesha mabadiliko ya tabianchi

Ikon. FNs bærekraftsmål nummer 13. Tegning avjordkloden. Tekst: Stoppe klimaendringene

Jinsi sisi wanadamu tunavyoishi tunaharibu tabianchi (hali ya hewa katika sehemu fulani kwa kipindi cha muda mrefu). Kunazidi kuwa na hali ya hewa yenye joto zaidi, barafu katika ncha ya dunia zinayeyuka, maji ya bahari yanazidi ongezeka na hali ya hewa mbaya zaidi inazidi kuwa kitu cha kawaida. Ni nchi maskini zaidi ambazo zimeathirika zaidi. Nchi zote lazima zishirikiane iliziweze kutoa gesi chafuzi kidogo. Pia, ni lazima tuzisaidie zile nchi ambazo zimeharibiwa na mabadiliko ya tabia nchi.


Maisha chini ya maji lazima yaangaliwe vizuri

Ikon. FNs bærekraftsmål nummer 14. Tegning av en fisk som svømmer. Tekst: Livet i havet.

Maisha duniani yanategemea bahari. Hali joto, mikondo ya bahari na maisha ndani ya bahari yanatuwezesha sisi binadamu kuishi duniani. Kwa hiyo ni lazima tulinde maisha ndani ya baharini, badala ya kutupa takataka na kuchafua.


Maisha ardhini lazima yaangaliwe vizuri

Ikon. FNs bærekraftsmål nummer 15. Tegning av et tre og noen fugler som flyr. Tekst: Livet på land

Eneo kubwa la dunia ni misitu. Msitu ni makazi ya idadi kubwa ya wanyama, na chanzo cha chakula kwa wanyama na watu. Ili sasa tutunze maisha ya ardhini (sehemu ya juu ya dunia tunaposihi), ni lazima tulinde misitu ya mvua, tupande miti mingi na tuhakikishe kwamba majangwa (eneo kubwa lenye mchanga mwingi) duniani hayawi makubwa. Ni lazima pia tulinde na kutunza viumbe vilivyo hatarini kutoweka.


Lazima kuwe na amani na haki duniani kote

Ikon. FNs bærekraftsmål nummer 16. Tegning av en hvit due som har en kvist i nebbet og sitter på en hammer. Tekst: Fred, rettferdighet og velfungerende institusjonerog

Bila amani na haki, haiwezekani kujenga maendeleo endelevu. Leo, watu wengi zaidi wanakimbia sehemu wanapokaa kuliko ilivyokuwa zamani. Ili kufikia lengo la amani na haki dunia, lazima ziundwe jamii zenye amani na zinazomjali kila mtu.


Nchi tajiri na masikini lazima zishirikiane

Ikon. FNs bærekraftsmål nummer 17. Tegning mange ringer som delvis overlapper hverandre. Tekst: Samarbeid for å nå målene-

Ili nchi zote ziweze kufikia malengo endelevu, ushirikiano ni muhimu. Mamlaka/uongozi, kampuni na raia/wananchi wote lazima washirikiane katika nchi zao na nchi zingine. Umoja wa Mataifa unaamini kuwa juhudi hizo za pamoja zenye malengo yaliyo wazi huleta majibu/matokeo.