Kjærlighet og seksualitet: Upendo na tendo la ndoa (mapenzi)
Upendo ni kuwa na furaha juu ya kitu fulani. Watu walio wengi wana mtu wanayemfurahia. Inaweza kuwa wazazi, ndugu ama rafiki. Pia kuna kile kinachoitwa upendo wa kimapenzi, ambao mtu anaojihisi au anajisikia kuwa na mpenzi ama mwenza wa ndoa.

Mtazamo juu ya upendo wa kimapenzi unatofautiana kati ya nchi na tamaduni tofauti. Pia kuna utofauti mkubwa ni jinsi gani wapenzi wanavyo tafutana na kukutana na kuwa pamoja. Sehemu nyingine ni wazazi ndio wanaowatafutia watoto wenza wao (mke au mume). Hii inaitwa ndoa au mahusiano ya kupangwa.
Wazazi wengine wanawapa nafasi watoto wao ya kuchagua ni nani wanahitaji kuoana nae, hivyo watoto wanachagua wenyewe kuwa ni nani wanayempenda zaidi. Sehemu nyingine wazazi wanawaamulia na bila ya kuwauliza watoto wao. Hii hairuhusiwi kumlazimisha mtu aweze kuoa au kuolewa ndani ya Norwei, lakini inaruhusiwa kutoa ushauri au mapendekezo kama watoto wao wanahitaji.

Ndani ya Norwei ni kawaida mtu kutafuta yeye mwenyewe mtu wa kuoana nae. Ni kawaida kuwa na wapenzi wengi kabla ya mtu kufanya uamuzi wa kufunga ndoa. Wengi wanahamia na kuishi kwa pamoja kabla ya kuoana. Inaitwa mahusiano ya kuishi pamoja bila ndoa. Robo ya watu wanaoishi pamoja hawaoani kabisa, lakini wanaishi pamoja na mara nyingi wanakuwa na watoto.

Pale mvulana na msichana wanapopendana tunaita wapenzi wa jinsia tofauti (heterofili). Lakini watu wawili wa jinsia moja wanapopendana kimapenzi tunaita kitendo cha ushoga au usagaji (homofili).
Katika nchi nyingine kuwa shoga au kuhusika na kitendo cha mapenzi ya jinsia moja hairuhusiwi na unaweza kuadhibiwa na hata kuuawa kama unaishi na kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Na katika dini fulani wanasema kuwa kujihusisha au kushiriki mapenzi ya jinsia moja ni makosa.
Ndani ya Norwei mtu anaweza kuishi pamoja na mtu yoyote anayemtaka. Hairuhusiwi kuwatenga au kuwabagua wapenzi wa jinsia moja, na wapenzi wa jinsia moja wanaweza kuoana kama ilivyo kwa wapenzi wa jinsia tofauti.

Kufanya mapenzi au kukutana kimwili ni jambo la kawaida na ni sehemu ya uhusiano wa kimapenzi. Ni kitu kizuri na cha kibinafsi ambacho watu wawili wanaweza kushiriki. Lakini hata ikiwa uko kwenye uhusiano, kila wakati unaamua juu ya kushiriki katika tendo la ndoa wewe mwenyewe. Hii ina maana kwamba unaamua kama unataka kujaribu kufanya mapenzi na nani na unayetaka kuwa nae. Hakuna mtu mwingine, sio wazazi, Mwenza wako au mpenzi, anaruhusiwa kuamua juu ya uhusiano wako wa kijinsia.

Kitendo cha kufanya mapenzi bila ya wewe kusema ndio tunaita ubakaji au kuingiliwa kimwili kinguvu. Na hii hairuhusiwi Norwei na unaweza pewa adhabu ya kufungwa gerezani. Pia hairuhusiwi kugusa au kuwagusa gusa wengine bila wewe kupewa ruhusa na mwengine kumfanyia hivyo. Ikiwa una shaka kama ni sawa kumgusa ama kuwa karibu nae sana kwa kumpapasa, unaweza kumuuliza.

Orodha ya maneno
Ndoa ya kupangwa – familia inachagua mume ama mke kwa watoto wao.
Kuishi pamoja – kuishi pamoja bila ya kuoana
Mapenzi ya jinsia tofauti – Kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu wa jinsia ya tofauti.
Mapenzi ya jinsia moja – Kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu wa jinsia moja inayofanana.
Kubaka – kulazimisha kufanya Mapenzi au kuingiliwa kimwili kinguvu.
Tekst og bilde er gjengitt og oversatt med tiltatelse fra Bergen kommune og zmekk.no