Lucia
Sikukuu ya Lucia inasherekewa siku ya tarehe 13 mwezi wa kumi na mbili. Nchini Norway siku hii inahusishwa na historia mbili. Historia kuhusu Lussi anaetisha na ile ya mtakatifu Lucia.
Lussi anaetisha
Zamani watu walikuwa wakiamini usiku wa tarehe 12 na 13 mwezi wa kumi na mbili ulikuwa ndio usiku mrefu zaidi katika mwaka. Usiku huo ulikuwa unaitwa usiku mrefu wa Lussi ama usiku wa Lussi. Kwa sasa tunajua kuwa usiku mrefu zaidi katika mwaka ni kwenye tarehe 21 mwezi wa kumi na mbili.
Watu waliamini kwamba usiku mrefu wa Lussi ulikuwa ni wa maajabu. watu waliamini kuwa wanyama waliweza kuzungumza na wenzao katika usiku huo. Usiku mrefu wa Lussi ulianzia mwanzoni mwa kipindi cha krismasi au (sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu). Walikuwa wanaelezewa kuwa Lussi alikuwa ni wa maajabu na mwenye umbo jeusi. Lussi alifuatilia ikiwa wote walikuwa vizuri na maendeleo ya maandalizi ya sikukuu ya krismasi. Kama kazi hazijafanyika basi alikuwa anaweza kuja na kuwatisha watu.
Kama mtu alikuwa nje wakati wa usiku mrefu wa Lussi, Lussi alikuwa anaweza kukuchua. Ndio maana watu walikuwa wanajiweka ndani katika usiku mrefu wa Lussi na kuangalia kuwa kazi za kufanya mpaka sikukuu ya krismasi imeanza. Moja ya kazi au mazoezi yalikuwa ni kuoka mikate au keki. Hivyo walitumia viungo vya safran au manjano ili mikate au vitu vinavyookwa viwe na rangi nzuri ya njano . Rangi ya njano ilikuwa inawakumbusha kuhusu mwanga au mwangaza uliokua umewashwa, katika wakati huo wa giza la usiku mrefu wa Lussi. Ile rangi ya njano pia ilikuwa inawakumbusha wote kuwa kipindi cha giza karibia kitakwisha na siku zitaanza kuwa na mwangaza zaidi tena.
Leo hii watu wanaoka mikate ya sukari yenye viungo vya safrani ama manjano katika siku ya Lucia tarehe 13 mwezi wa kumi na mbili. Mikate ya sukari au skonsi hizi zinapambwa na zabibu zilizokauka na zinaitwa skonsi za Lusia kwa kinorwei “lussekatter”.

Nyimbo ya Lucia
Mazoezi ya maswali ya kuandika ya maandishi kuhusu Lussi
- Elezea ni nini usiku mrefu wa Lussi ?
- Elezea Lussi ni nani?
- Kwa nini watu walikuwa wanamuogopa Lussi?
- Chora, ni jinsi gani unazania Lussi anavyoonekana.
- Lini ni usiku mrefu katika nchi za kaskazini mwa ulaya?
- Mikate au Skonsi iliyookwa siku ya Lucia inaitwaje?
- Rangi inayowakilishwa katika unga wa skonsi au mikate ya Lucia zina maanisha nini?
Mtakatifu Lucia
Tarehe 13 mwezi wa kumi na mbili inasherekewa siku ya Lucia, ni kwajili ya kukumbuka kuhusu mtakatifu Lucia. Jina Lucia linatoka katika lugha ya kilatini “lux” inayomaanisha mwanga au mwangaza.
Lucia aliishi kipindi cha miaka ya 300 katika mji uitwao Sicilia nchini Italia. Yeye alikuwa mkristo na anaeamini juu ya Yesu kristu. Katika kipindi hicho wale waliokuwa wakristo walifatiliwa na warumi. Lucia alitakiwa kuoelewa au kuozeshwa kwa mwanaume tajiri wa kirumi, lakini yeye alikataa kuolewa. Yule mwanaume tajiri wa kirumi alikasirika na kuumizwa. Hivyo akawaambia watu waliokuwa wanaongoza na kuamua nchini kuwa Lucia alikuwa mkristo. Kwahiyo Lucia aliadhibiwa na Warumi na akafa kifo cha kishahidi kutokana na dini au imani yake.
Mtu anaekufa kwa sababu ya ushahidi wa kidini ni mtu anayekufa kutokana na imani yake. Kuna hadithi nyingi kuhusu mambo mazuri ya Lucia. Lucia baadae akawa mtakatifu katika ukristo. Kipindi kile ambacho Lucia alikuwa anaishi ilibidi watu waishi kwa kujificha. Wengine walijificha kwenye mashimo yaliyokuwa chini ya ardhi yenye giza. Waliweka mishumaa kwenye vichwa vyao ili kuangaza ndani ya mashimo. Wakristo walimfikiria Lucia kama msichana ambaye alionyesha njia ya imani katika wakati wa giza

Sehemu nyingine siku ya Lucia inasherekewa katika mashule na kwenye chekechea au shule za watoto wadogo. Watoto wanatembea kwa kufuatana kwa maandamano na wanavaa nguo nyeupe. Ni kawaida kwa mtu mmoja kutembea wa kwanza mbele akiwa na taji la mishumaa inayowaka kichwani. Wengine wakimfuatia, wakiwa wamebeba mishumaa au nyota mikononi mwao huku wakiimba nyimbo za Lucia. Wazazi na wageni wengine mara nyingi wanaalikwa kwajili ya kuangalia matembezi ya maandamano au msafara wa lucia. Baadae wanakula mikate au maandazi ya kuoka ya lucia pamoja na watoto.
Video inayoonyesha maandamano ya lucia.
Kazi ya maswali kuhusu maandishi ya Mtakatifu Lucia
- Tarehe 13 mwezi wa kumi na mbili wanasherekea nini? Elezea;
- Nani anakumbukwa katika siku ya Lucia?
- Ni jinsi gani siku hiyo inakumbukwa au inasherekewa hapa Norwei?
- Jina Lucia lina maanisha nini?
- Je unaijua siku nyingine ambayo watu wanasherekea kuhusu mtu ambae aliwahi kuishi?
