Id al-adha// Id al-adha

Id al-Adha ni sherehe kwa Waislamu duniani kote. Sherehe hiyo pia inaitwa Eid kubwa au Sikukuu ya Sadaka. Sherehe ya Eid inaadhimisha mwisho wa ibada ya Hija mjini Makka. Tarehe inabadilika mwaka hadi mwaka. Makka ni mji ndani ya nchi ya Saudi Arabia na mahali patakatifu zaidi katika Uislamu.

Hija, Safari ya hija Makka, ni moja ya nguzo tano ambazo Uislamu umejengwa nazo. Waislamu wanaoweza kufanya hivyo lazima waende kuhiji mara moja katika maisha yao. Kila mwaka kati ya Waislamu milioni tatu hadi nne husafiri kwenda Makka.

Shughuli moja inayofanywa na Waislamu wanapokuwa kwenye Hijja ni kutembea mizunguko saba kuzunguka Al-Kaaba. Kaba ni jiwe takatifu, kulingana na dini ya kiislamu, jiwe lililetwa duniani na malaika Jibril/Gabrieli.

Katika sikukuu ya Id al-Adha, Waislamu mara nyingi hula chakula cha sikukuu kikiwa na nyama ya mbuzi, kondoo au ng’ombe.Ni lazima wamkumbuke nabii Ibrahimu ambaye alikuwa tayari kumtoa mwanawe dhabihu ili kuonyesha utii wake kwa Mungu.

Wakati wa Eid al-Adha, Waislamu huvaa nguo nzuri. Wanakula chakula kizuri na familia na marafiki. Wengi huomba na kupeana kadi za sikukuu ya Eid au zawadi. Katika Eid al-Adha, wanatakiana “id mubarak” ambayo inamaanisha Eid njema.

Finn ut mer om Islam