Id al-fitr // Id al-fitr
Id al-fitr mara nyingi huitwa sikukuu ya idd / Eid. Inasherekewa kuwa kile kipindi cha kufunga katika mwaka kimekwisha. Mwezi wa kufunga au mfungo unaitwa Ramadhani kwa Waislamu wote, na watu wazima wote wanaweza kufunga. Wale wanaofunga hawali chakula kuanzia jua linapoanza kutoka hadi jua linapo zama (magharibi au jioni). Katika Ramadhani, ni muhimu kufikiria jinsi tunavyoweza kuwa wema na wazuri kwa kila mmoja wetu. Katika Idd, tunamshukuru Mungu kwa kutupa nguvu ya kutekeleza mfungo au kufunga. Sherehe huanza na maombi ya ibada ya pamoja katika msikiti.
Katika sikukuu ya Iddi, ni kawaida kuwa pamoja na familia na marafiki. Sherehe ya Iddi ni sikukuu ya watoto. Mara nyingi watoto hupokea zawadi au pesa kutoka kwa familia. Zawadi hizo zinaitwa iddi. Ni kawaida kujipendezesha kwa kuvaa nguo nzuri. Watu wengi hupamba mikono yao na hina /henna.
Kabla ya sherehe ya Iddi, ni kawaida kwa wale ambao wana uwezo kutoa zakat al-fitr. Pesa zitatolewa kwa wale wenye uhitaji ili waweze kununua chakula cha sherehe, zawadi au nguo mpya kwa ajili ya sherehe hii kubwa.
Chakula ni sehemu muhimu ya sherehe ya sikukuu ya Iddi/ Eid. Familia na marafiki hukusanyika kwa ajili ya chakula cha pamoja cha sherehe, wanapata chakula kizuri na vitu vya kula vilivyo vitamu (pipi). Chakula katika meza huwa ni tofauti kati ya familia moja hadi familia nyingine.
Ni kawaida kusalimiana “Id Mubarak” ambayo ina maana unamtakia mtu sikukuu yenye baraka. Watu wengi wanapeana au kutumiana kadi za sikukuu ya iddi / Eid.