Ubudha

Denne teksten finnes på flere språk. Tanken er at teksten skal være et supplement til andre læremidler og andre aktiviteter i opplæringen. Det er altså ikke meningen at disse ressursene skal stå alene, men at de kan brukes i innledning til arbeid med temaet.

Teksten kan, for eksempel, brukes sammen med tospråklig lærer for å aktivere elevenes kunnskaper om temaet, og å bidra til at eleven lærer fagspråk.

Ubudha ulitokea Kaskazini mwa India zaidi ya miaka 2500.

Dini ilianzishwa na mwanaume anaeitwa Siddharta Gautama.

Illustrasjon som viser Buddha som liten gutt med en gloria rundt hodet. Det er i en hage med trær og lotusblomster. Rundt han står damer i fargerike klær
Buddha alizaliwa kama mtoto wa kiume wa mfalme aliishi maisha ya kitajiri na kulindwa. Kutokana na utamaduni wa kibudha, Budha aliweza kutembea alipozaliwa, na alipotembea hatua saba za kwanza paliota maua ya lotus katika sehemu za alama za nyayo za miguu yake.

Budha

Siddharta Gautama alikuwa ni mtoto wa kiume wa mfalme. Huyu alitokea katika familia ya kitajiri na aliishi maisha mazuri kwenye jumba la kifalme. Siku moja alipotoka nje ya jumba la kifalme alipata kuona mtu aliyekuwa mgonjwa, mtu mzee, mtu alie kufa /maiti na mtu aliyejinyima raha na kufunga kwa sababu ya dini. Mtu aliyejinyima raha ni mtu aliyechagua kuishi maisha rahisi. Kile mtoto wa kiume wa mfalme alichokiona nje, kilimfanya aamue kwa kuhama kwenye nyumba ya kifalme, mke wake na mtoto wake aliyezaliwa. Yeye alitaka kuishi kama mtu wa kujinyima raha . Watu wa kujinyima raha wanamaanisha wanaweza kuwa wenye busara na kuelewa zaidi kama wataishi maisha rahisi. Siddharta aliwatembelea watu wengi wa kujinyima raha na kujifunza zaidi kutoka kwao. Yeye alifunga kwa kutokula Chakula na alikaa na kutafakari kwa utulivu sana.

Kutafakari ina maanisha unakaa kimya kwa utulivu na kujaribu kutofikiria kitu chochote. Baada ya kuishi kama mtu wa kujinyima raha kwa miaka 6, Siddharta alifikiria bado hajapata jibu, yeye hakuwa mtu mwenye hekima au busara sana. Ndipo akaamua kukaa chini ya mti na kutosimama tena juu kabla hajakuwa mtu mwenye hekima. Baada ya kukaa chini ya mti kwa siku nne, kwa ghafla Siddharta akaelewa ni jinsi gani dunia ilivyo .”Nimepata uhuru,’ aliwaza. Sasa akawa Buddha. Buddha ni neno la Kihindi linalomaanisha ” Yule mwenye kuelewa”

Malt illustrasjon av Buddha som sitter i lotusstilling under et tre
Baada ya kukaa chini ya mti kwa siku nne, kwa ghafla Siddharta akaelewa jinsi gani dunia ilivyo na alipewa taarifa. Akawa Budha.

Imani

Budha hakuwa Mungu, lakini alikuwa mtu mwenye hekima au akili nyingi na kuelewa vitu sana. Budha aliwafundisha watu kwa nini ni muhimu kuwa wapole na wakweli kwenye maisha. Baada ya kifo cha Buddha, mafundisho yake yameendelea kuishi. Haya ndiyo mafundisho tunayoyajua leo kama Ubudha. Mafundisho pia yanaitwa dharma.

En illustrasjon av Buddha som forteller sin vidsom til andre.
Budha alikuwa mwalimu na kuzungumza na watu jinsi gani wao pia wanaweza kupata taarifa na kuishi maisha mazuri.

Wabudha wanaamini kwenye kuzaliwa upya tena. Mbudha anamaanisha kuwa utazaliwa tena pale utakapo kufa. Kile utachofanya katika maisha ya sasa yatamua jinsi gani maisha yako ya baadae yatakuwa. Kama hauko vizuri katika maisha haya, utapata wakati mgumu kwenye maisha yajayo. Mafundiho haya yanaitwa karma.

Budha aliwaeleza watu kwamba kuna matatizo mengi duniani, kuna mateso mengi na watu wengi ambao hawapo vizuri. Budha pia alisema kuna uwezekano wa kufanya kitu dhidi ya mateso. Binadamu wanaweza kufanyia kazi kujenga uelewa zaidi, kuwa wapole, kuacha chuki, kutofikiria vitu vinavyoleta maumivu, usiwe na tamaa daima ya kutaka zaidi. Ikiwa watu wanaweza kufanya hivi, wanaweza kuwa huru na kuwa na wakati mzuri. Huu uhuru unaitwa Nirvana. Nirvana ni ukombozi kamili kutoka katika mateso na kuzaliwa upya. Ni hali ya furaha, maelewano, uhuru kamili na uwazi usioelezeka.

To hender som holdes med håndflatene mot hvernadre. Armene løftes opp og hendene holdes foran solen, slik at noen solstråler lyser igjennom fingrene.
Katika ubudha malengo ni kufikia nirvana. Kuwa na maisha mazuri yenye maelewano na uwazi .

Ukweli 4 mtukufu

Mafundisho ya budha yanaweza kuelezewa kwa kifupi kupitia sentensi nne za mafundisho. Hizi zinahusu kwa nini kuna mateso mengi kwa watu na jinsi gani ya kubadilisha haya .

  1. Kila kitu kina maumivu ama mateso
  2. Kuna mateso kwa sababu watu ni wachoyo au hawatosheki. Watu siku zote /daima wanataka vitu zaidi.
  3. Ikiwa watu wataacha kuwa na tamaa na kutaka vitu zaidi katika maisha yao, maumivu na mateso yatatoweka. Kama mtu anataka kuachana au kufikia mwisho wa yote yanoleta maumivu, ni lazima mtu afuate njia 8 zilizogawanyika.

Kama sisi watu tutafanyia kazi na kuelewa zaidi, tutakuwa na maisha mazuri na mateso yanaweza kuisha.

Njia nane zilizogawanyika

Budha alisema: Watu lazima waelewe nini kisichokuwa vizuri katika maisha yao kabla ya “kurekebisha” maisha yao. Budha alisema pia watu lazima wafuate zile njia 8 ili kufikia nirvana.

  1. Kuwa na ufahamu sahihi. Elewa au fahamu zile Kweli takatifu 4 bora, kuhusu sheria ya Karma na Kuzaliwa Upya..
  2. Kuwa na mawazo sahihi. Fikiria kwa upendo juu ya watu wengine, toa bila kufikiria kuwa utapata chochote kama malipo.
  3. Kuwa na maelezo au ushuhuda sahihi. Sema ukweli na usiseme uwongo, umbea au kusengenya.
  4. Fanya vitu vilivyo sawa. fuata hizi kanuni tano za kuishi kwenye ubudha
    • kujiepusha na kuua (kutoua).
    • kujiepusha na kuiba (kutoiba).
    • Kujiepusha na kufanya mapenzi na mtu mwingine asiyempenzi wako (kutofanya mapenzi na mtu asiye eke au mume wako).
    • Kujiepusha na kudanganya (kutosema uongo).
    • Kujiepusha na kulewa (kutolewa).
  5. Kuwa na njia sahihi ya maisha. Kuwa na kazi ya ukweli/uadilifu, kutopata pesa kwa njia mbaya, kwa mfano; kuiba, kuua au kudanganya watu wengine..
  6. Kuwa na juhudi sahihi. Fanya kazi kwa bidii na ujitahidi kuwa mtu bora na mwenye busara.
  7. Kuwa na tahadhari sahihi. Jizoeshe kutofikiria mambo mengine unapofanya jambo fulani, bali fikiria kile unachofanya kwa wakati huu.
  8. Kuwa na umakini au ufatiliaji wa kimawazo sahihi. Jifunze kuwa na amani kichwani na moyoni mwako na kuwa mwenye nguvu kichwani na moyoni.
Et tegnet hjul med åtte eiker som illustrerer dhramahjulet i Buddhismen
Gurudumu la Tairi la dharma ni alama ya kawaida katika ubudha. Hizi ni Sehemu nane za kuzishika zinaashiria njia nane kuelekea nirvana.

Maandishi na alama

Kuna maandiko mengi matakatifu au maandishi katika ubudha. Maandishi hayo yanahusu maisha ya Budha na mafundisho yake. Mafundisho ya Buddha yalisimuliwa kwanza kwa mdomo kutoka kwa mwalimu hadi kwa mwanafunzi, lakini baadae ikawa ni muhimu kuandika maandishi ili mafundisho yasije kupotea.

tibet monk buddhist book prayers written language
Watawa wa kiume na watawa wakike wanasoma mara nyingi maandiko kama sehemu ya kupata mafundisho kutoka kwa Budha.

Kwenye mahekalu ya ubudha mara nyingi huwa na sanamu kubwa za Budha, na nyingi ya sanamu hizo zina thamani kubwa sana katika kazi ya sanaa.

The Giant Golden Buddha in Wat Paknam Phasi Charoen Temple in Phasi Charoen district, Bangkok urban city, Thailand.
Picha inaonyesha budha mkubwa wa rangi ya dhahabu kwenye hekalu katika jiji la Bangkok nchini Thailand.

¨.

Katika mahekalu mengi kuna madhabahu na sanamu za budha. Ibada ya tampico la puja mara nyingi hufanywa huko, ambayo ni ibada ya budha kwa njia ya kuimba, kutafakari na kutoa maua na ubani au uvumba.

Bilde viser et alter i et tempel med mange blomster og buddhastauer og bilder.
Picha inaonesha madhabahu ndani ya hekalu kukiwa na maua mengi na sanamu za kibudha na picha.

Wabudha wengi wana kitu cha kutengenezwa cha kufanana na budha nyumbani. Wanawasha mishumaa na kuweka maua mbele ya sanamu la budha. Baadhi ya wabudha wanakaa kwa utulivu na kutafakari kila siku.

Bilde av et budddhistisk tempel på en solfylt dag med blå himmel
Picha inaonesha hekalu la zamani la kibudha kutoka Shanghai,China .

Watawa wa kiume na watawa wa kike

Watawa wa kiume na watawa wa kike ni wataalamu au wanaojua zaidi kuhusu ubudha. Wanasoma sana katika maandiko matakatifu. Wanatafakari na kufundisha mafundisho ya budha. Hawana vitu vingi, wapo na vitu vile wanavyovihitaji tu. Wanaishi kwa chakula na zawadi wanazopata kutoka kwa watu.

Bilde av to munker ikledd orange klær
Picha inaonesha watawa wawili wakiume wakisalimiana katika monasteri ya kibudha huko Asia.

Jifunze zaidi kuhusu ubudha


  • Tekstene er utviklet av Veilederkorpset i Stavanger og etter avtale tilrettelagt, bearbeidet og oversatt av morsmål.no
  • Alle bilder er hentet fra Adobe Stock