Islam // Uislamu
Uislamu ni dini iliyo ndogo zaidi kati ya dini tatu zilizoanzia mashariki ya kati (mashariki ya kati ni eneo zinapopatikana nchi zilizopo magharibi ya bara la Asia na kaskazini mashariki mwa bara la Afrika). Uyahudi na ukristo ni dini mbili nyingine zilizoanzia mashariki ya kati. Uislamu unafanana na Uyahudi na ukristo katika kuamini Mungu alie mmoja. Hivyo zinaitwa dini zinazoamini katika Mungu alie mmoja.

Uislamu ni dini ya pili inayofuata kwa ukubwa duniani baada ya dini ya ukristo (ukristu inaanza, alafu inafata uislamu). Kuna karibu watu bilioni moja nukta saba (bilioni 1.7) duniani ambao wana amini katika uislamu. Watu wanaoamini katika uislamu tunawaita waislamu. Umoja wa waislamu kwa kiarabu unaitwa umma. Umma unagawanywa katika makundi mawili makuu. Kuna waislamu wasuni na waislamu washia. Mtume Muhammad alianzisha uislamu karibia miaka 610 baada ya Yesu kristo. Ilitokea katika mji aliozaliwa wa Maka. Mji wa Maka upo nchini Saudia Arabia. Mohammed alikufa mwaka 632 baada ya kristu.
Korani na hadithi
Korani ni kitabu muhimu kitakatifu katika uislamu. Kwa mujibu wa uislamu, korani ina mafunuo ambayo mtume Muhammad alipokea toka kwa Mungu. Korani hapo mwanzoni iliandikwa kwa kiarabu.

Korani ina sura 114. Sura kwa kiasi zimepangwa kuwa kuangalia ni ndefu kiasi gani. Zile ndefu zinakuwa mwanzo na fupi zipo mwishoni. Sura ya kwanza ni ya kipekee, ipo na sala fupi ya kuanzia ya al-fatiha. Waislamu wanaibusu Korani kabla ya kuisoma.
Katika miaka mia moja iliyofuata baada ya kufa mtume Muhammad, maelezo ya kile alichosema ama kufanya yaliandikwa kwenye vitabu vinavyoitwa hadithi. Korani na hadithi kwa pamoja vinaonesha nini ni sawa na njia nzuri ya kuishi kwa waislamu.
Nguzo tano
Uislamu ni dini ya sheria. Hii inamaanisha sheria na taratibu zina amua nini kilicho sawa na si sawa, na nini muislamu atafanya. Hii imeelezwa katika nguzo tano za uislamu.
Kukiri imani (Shahada)
Kukiri imani au shahada ni nguzo ya kwanza kwenye uislamu. Kwa kiarabu ni «Ashhadw ana la ila Allah wa ashhadw ana Mohammad rasol Allah». kwa kiswahili ina maana “hakuna Mungu ila Allah, Muhammad ni mtume wa Allah”

Sala
Nguzo nyingine ni sala au maombi . Muislamu anatakiwa kumuomba Mungu mara tano katika siku moja. Waislamu wana sali juu ya mkeka au zuria, mkeka huo wa kusalia ambao unatandikwa chini unawezesha mtu kuwa katika muelekeo ulipo mji wa Maka.

Ni muhimu kuwa msafi kabla ya kuomba. Sala zipo kwa kiarabu na zina maandiko toka kwenye Korani. Wakati wa kuomba mwili hugeuka katika muelekeo maalumu. Mtu anasimama, anainama, anaenda chini kupiga magoti huku uso na mikono ikiwa chini na anakaa. Sala ya ijumaa ni moja ya sala tano za kwenye siku, lakini ukiongezea kwenye sala hii ya pamoja, pia husikilizwa mahubiri. Anae ongoza sala na mahubiri anaitwa imamu.
Zaka
Nguzo ya tatu ni zaka au sehemu ya mapato ya mtu anayopaswa kutoa. Zaka ni kiasi unacholipa kutokana na kiasi gani cha pesa, mapambo na vitu mtu anavyomiliki. Pesa wanapewa watu wenye uhitaji.
Kufunga au kutokula chakula kwa masaa
Kufunga ni nguzo ya nne. Kufunga ni kwenye mwezi wa Ramadhani, ina maanisha mtu hawezi kula au kunywa kuanzia wakati jua linatoka hadi jua linapo zama magharibi. Watoto hawahitaji kufunga. Baada ya jua kuzama familia inakuwa pamoja kwa chakula cha jioni kinachoitwa futari (iftar). Wakati wa ramadhani ni muhimu kuonesha shukrani kwa kile ulicho nacho na kuwa na huruma zaidi kwa wale ambao hawana vingi.
Safari ya sehemu takatifu
Nguzo ya tano ni kufanya safari ya kwenda sehemu takatifu (kuhiji) katika mji wa Maka. Lengo ni kuhiji. Kuna taratibu kadhaa zinazohusiana na kufanya safari ya kwenda sehemu takatifu (hija). Taratibu zote lazima zifanye ili ihesabike mtu amefanya safari ya kwenda sehemu takatifu (Kuhiji) kihalali. Moja ya taratibu kwa mfano ni kutembea mara saba kuzungunga Kaaba. Kaaba ni takatifu kwa sababu ina lile jiwe jeusi. Kwa mujibu wa uislamu jiwe hilo lina asili ya mbinguni na lililetwa duniani na malaika Gabrieli.
Muislamu anatakiwa kwenda kuhiji mara moja katika maisha yake, kama anauwezo. Kila mwaka kati ya waislamu milioni tatu hadi nne wanasafiri kwenda mji wa Maka.

Kaaba iko ndani ya msikiti mkuu ndani ya Maka Picha : Pixabay, Konevi