Jødisk påske // Pasaka ya Kiyahudi-Pesaki

Denne teksten finnes på flere språk. Tanken er at teksten skal være et supplement til andre læremidler og andre aktiviteter i opplæringen. Det er altså ikke meningen at disse ressursene skal stå alene, men at de kan brukes i innledning til arbeid med temaet.

Teksten kan, for eksempel, brukes sammen med tospråklig lærer for å aktivere elevenes kunnskaper om temaet, og å bidra til at eleven lærer fagspråk.

Yesu alipoingia Yerusalemu kwa farasi siku ya saba (jumapili) ya mitende, yeye na wanafunzi wake walikuwa wanaenda kusherekea pasaka ya kiyahudi iitwayo pesaki (pesach kwa ki norwe). Pesach kwa kinorwe ni pasaka ya Wayahudi na inawakumbusha kipindi waisraeli walipokuwa watumwa Misri chini ya Farao. 

illustrasjon av av slaveriet i Egypt i bibelsk tid

Historia ya Musa 

Kwenye biblia agano la kale kitabu cha kwanza cha Musa, tunasoma kwamba Waisraeli walikaribishwa Misri. Lakini baada ya miaka mingi ikawa Farao (aliyekuwa kiongozi Misri) ana wasiwasi kuwa waisraeli watakuwa wengi. Kwa hiyo waisraeli wakafanywa watumwa na Farao akaamuru watoto wote wa kiume waliozaliwa wauliwe. Mama yake Musa hakutaka mtoto wake auliwe. Akamuweka Musa kwenye kikapu na kukiweka kwenye mto Nile. Alitumaini kuna mtu atamchukua na kumuangalia vizuri. Mtoto wa kike wa Farao alikiona kikapu na kukichukua pamoja na mtoto. Alimtunza mtoto  vizuri. Musa alikulia kwenye familia ya Farao. 

Baby Moses dropped in the river with pharaoh's daughter in the distance.

Musa alipokua mkubwa, Mungu alimtokea Musa katika kichaka (ambayo ni sehemu yenye miti midogo mifupi iliyo pamoja na majani) kichaka kilichokuwa kinawaka moto. Mungu alimwambia atawasaidia watumwa Misri na kwamba Musa yeye ni Mwiisraeli. Ilikuwa ni watu wake Musa wanaoteseka kwenye utumwa chini ya mtu ambae Musa anamuita baba. Mungu alimwambia Musa kwamba amuombe Farao awaachilie watumwa. Musa alipaswa kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri na kuwaingiza katika nchi nyingine iliyoitwa nchi ya Kanani.  

Biblical vector illustration series, Moses and the burning bush

Mapigo kumi na pasaka ya kwanza

Musa alikwenda kwa Farao iliawaachie huru Waisraeli, lakini Farao alikataa. Kisha Mungu akatuma mapigo kumi juu ya Misri, yakiwemo ugonjwa wa tauni, giza na nzige. Hatimaye likaja pigo baya kuliko yote. Malaika wa Bwana alipita katika mitaa ya mji na kuwaua watoto wa kwanza kuzaliwa katika kila familia. 

Hapo kabla Waisraeli walikuwa wamepokea onyo kutoka kwa Mungu kupitia Musa. Kwa hiyo walipaswa kujiokoa dhidi ya malaika wa kifo kwa kuchinja mwana kondoo na kupaka damu yake kwenye nguzo za milango (miimo). Malaika alipita karibu na nyumba hizo ambapo kulikuwa na damu kwenye nguzo za milango (miimo). Lakini aliingia katika kila nyumba nyingine isiyokuwa na damu. Ili kufanya pigo hilo la kumi, Farao alilazimika kuwaruhusu Waisraeli watoke Misri. Ni tukio hili ambalo linaunda kuanzishwa kwa Pasaka ya Kiyahudi.

Wayahudi wana sheherekea vipi pasaka?

Jioni ya kwanza ya sikukuu ya pasaka ya wayahudi wanakula  manna chakula cha pasaka cha Wayahudi kiitwacho sedermåltidet (kwa kinorwe). Chakula ni kwa ajili ya kuwakumbusha kutoka kwao Misri. Chakula kinaanza kwa kubariki mvinyo (ambao ni kinywaji kinachotengenezwa kwa maji ya matunda ya zabibu).

Bilde av en gutt som leser en tekst fra en bok. Han sitter rundt er middagsbord med mange andre og det viser en jødisk høytid Pesah

Sahani ya manna kwa kinorwe Sedertallerkenen ni sahani yenye vyakula vidogo vidogo ambavyo vina maana maalum. Mwanzoni mwa chakula huwasha wayahudi mshumaa, wanaoita mshumaa wa sabato.

Bilde av en tallerken med , egg, salat, utrer, kylling og brød på
En sedertallerken
  1. Matzah ni mkate usiotiwa chachu, yaani, mkate ambao haujaumuka. Wayahudi walipolazimika kutoroka Misri hawakuwa na muda wa kutia chachu na kuacha mkate uumuke wao walioka (kupika kwa kuchoma).
  2. Charoset ni mchanganyiko wa apple, divai (juisi ya matunda ya zabibu ambayo ni mpya na bado haijachachuka) na karanga. Inawakumbusha mchanganyiko wa matofali ambao Wayahudi walitumia wakati walipokuwa watumwa, walilazimika kutumia wakati waki wajengea Wamisri..
  3. Zroah/Zeroa ni mguu wa kondoo, bawa la kuku au shingo ya kuku. Chakula hiki kinapaswa kuwa ishara ya dhabihu (dhabihu ni kitu ama mnyama anayetolewa kama sadaka) ya Pasaka. Sadaka ya Pasaka ilikuwa ni mwana kondoo aliyetolewa kama zawadi katika hekalu la Yerusalemu. Mwana kondoo alichomwa wakati hekalu likiharibiwa.
  4. Chazeret ni mmea mchungu ama saladi inayowakumbusha machungu waliyopitia Misri.
  5. Beytzah ni yai la kuchemsha linalomaanisha sadaka ya likizo, ni sadaka ya kuongezea ya pasaka iliyopelekwa pamoja hekaluni.
  6. Karpas ni persiller (majani yanafanana na korianda) iliyotiwa ndani ya maji ya chumvi, ili maji yafanane na machozi. Hii itawakumbusha Wayahudi machozi yaliyowatoka wakati walipokuwa watumwa Misri.
  7. Maji yenye chumvi (kwa ki norwe Saltvann) inaashiria machozi ya wayahudi ambapo persille (majani yanafanana na korianda) na yai.

Utaratibu wa matukio ya usiku wa chakula cha manna (seder) yameandikwa kwenye kitabu kinachoitwa Haggadah. Haggadaen ina mambo mengi,yakiwemo hadithi ya utumwa wa Wayahudi Misri, hadithi na maelezo jinsi seder inapaswa kufanywa.  

Bilde av et drikkebeger, en bok og flatt brød. Alle tre ting som brukes den første kvelden av den jødiske høytiden peasah.

Sherehe ya chakula cha  manna au Seder ni cha huzuni na cha furaha. Wanapaswa kukumbuka nyakati mbaya za Misri, lakini pia wanafurahi kwamba Wayahudi waliweza kutoroka kutoka utumwani.

kunstmosaikk som ilustrerer da moses delte havet slit av isralittene kunne gå tørre gjennom vannet