17. mai – Norges nasjonaldag // Tarehe 17 mwezi wa tano – Siku ya kitaifa ya Norwe
Tarehe 17 mwezi wa tano ni siku ya kitaifa ya Norwe. Tunasherekea Norwe kupata katiba/sheria yake tarehe 17-05-1814. Kabla ya mwaka 1814 Norwe ilikuwa sehemu/inayoongozwa na mfalme wa Denmark kwa miaka zaidi ya 400. Mfalme wa Denmark ndio aliyekuwa kiongozi wa juu zaidi na watu wa Norwe iliwabidi kufuata sheria zilizoamuliwa nchini Denmark. Katika mwaka 1814, Ulaya kulikuwa na vitu vingi vilivyotokea na wanorwe walitamani kuwa nchi huru na yenye sheria zake yenyewe.
Kuandikwa kwa Katiba Eidsvoll
Katika mwaka 1814 walikusanyika wanaume 112 katika mji wa Eidsvoll kwa ajili ya kuandika katiba ya Norwe. Watu hao walitoka sehemu mbalimbali ndani ya Norwe. Mkusanyiko huo wa wanaume wote uliitwa bunge, walitumia wiki sita kuandika katiba. Tarehe 17 mwezi wa tano ilimalizika na kusainiwa/kufinya na mfalme Christian Frederik, na ndio maana tarehe ya siku hiyo tunaiita sikukuu ya kitaifa Norway.

Tarehe 17 mwezi wa tano ni siku ya bendera
Tarehe 17 mwezi wa tano ni siku ambayo wanafunzi hawaendi shule na kwa watu wengi wanakuwa hawafanyi kazi. Ni siku maalumu/rasmi ya bendera, ina maana majengo yote yanayomilikiwa na serikali ama halmashauri lazima wapandishe bendera juu siku hiyo. Watu binafsi pia wana peperusha bendera tarehe 17 mwezi wa tano. Bendera ya Norwe ilitengenezwa mwaka 1821. Ina rangi zenye kumaanisha uhuru: nyekundu, nyeupe na bluu.
Msalaba unaashiria kuwa Norwe inapaswa kuwa nchi ya kikristo.

Nguo za sherehe
Ni kawaida kwa watu kujipamba na kuvaa nguo nzuri katika siku ya kitaifa. Watu wengi wanavaa nguo ya asili inayoitwa bunad ama mavazi mengine ya taifa. Kwenye tarehe 17 mwezi tano kunaandaliwa hotuba zinazotolewa katika mashule, bustani/mashamba madogo ama maeneo ya katikati ya jiji.
Maandamano ya watoto
Tarehe 17 mwezi wa tano inaitwa pia siku ya watoto. Kote nchini Norway watoto wa shuleni huandamana, wanapeperusha bendera, wanapiga kelele za kushangilia hurra na kuimba. vikundi vya watu/kwaya vinapiga mziki. Siku hiyo watu wengi huimba nyimbo ya taifa (Ndio, tunaipenda nchi yetu). Mashairi ya nyimbo ya taifa yaliandikwa na mshairi maarufu Bjørnstjerne Bjørnson mwaka 1859. Mwaka 1863 mtoto wa mjomba/binamu yake aitwaye Rikard Nordraak aliandika melodi ya nyimbo ya taifa.


Sherehe za vijana wanaokaribia kumaliza elimu ya sekondari ya juu (Russ)
Wanafunzi wa sekondari ya juu(videregående) wanasherekea kumaliza masomo yao ya sekondari ya juu. Baadhi yao wamesoma masomo shuleni kwa miaka 13. Wanavalia nguo zao za sherehe hizo (russedress). Kwenye nguo hizo huandikiana salamu na kalamu za wino mnene (tusj). Wanafunzi wa sekondari ya juu wanakuwa wanafanya sherehe nyingi ndani ya mwezi wa tano. Wengi wanakuwa na magari binafsi au mabasi, wanayo endesha huku wakipiga mziki kwa sauti ya juu. Wengi huwatania walimu wao na kuwaamsha mapema asubuhi siku ya tarehe 17 mwezi wa tano. Katika maeneo mengi wanafunzi wanaomaliza sekondari ya juu wanaandamana wakiwa wanacheza mziki, kuimba na kuonesha michoro yenye kufurahisha.
Familia ya mfalme
Mfalme wa Norwe anaitwa Mfalme Harald na malikia (mke wa mfalme) anaitwa malikia Sonja. Mfalme, malikia na familia ya kifalme kwa ujumla wanasimama barazani mwa jumba la kifalme kila tarehe 17 mwezi wa tano na kuwapungia mkono watoto wanaoandamana mjini Oslo.
Maandamano ya watoto yanapita na kuelekea juu katika mtaa mkuu uitwao Karl Johans gate. Maandamano yanapita katika jumba la kifalme, watoto wote na walimu wao wanapungia mkono familia ya kifalme na familia ya kifalme wanawapungia pia mkono. Kuna zaidi ya shule mia moja zinazoshiriki maandamano ya watoto Oslo.

Bilder i innlegget er hentet fra:
- Bilde 1: Maleriet heter Eidsvold 1814 og er malt av Oscar Wergeland. Kilde: Wikipedia.
- Bilde 2: Norges flagg.Vegard Ottervik,Pixabay
- Bilde 3: Barnetoget i Oslo foran slottet.Morten Johnsen, Wikipedia.
- Bilde 4: Russetog, Dmitry Valberg, Flicr. CC BY-NC-ND 2.0
- Bilde 5: Kongefamilien på balkongen på slottet. Shutterstock.