Rettstaten // Nchi inayofuata sheria

Denne teksten om Rettsstaten finnes på flere språk. Teksten er hentet fra Zmekk.no og oversatt til flere språk av morsmål.no eter avtale med Bergen kommune. Tanken er at teksten skal være et supplement til andre læremidler og andre aktiviteter i opplæringen. Det er altså ikke meningen at disse ressursene skal stå alene, men at de kan brukes i innledning til arbeid med temaet.

Teksten kan, for eksempel, brukes sammen med tospråklig lærer for å aktivere elevenes kunnskaper om temaet, og å bidra til at eleven lærer fagspråk.

Scroll nedover for å finne flere ressurser.

Zmekk.no

Nchi zote zina sheria na kanuni ambazo lazima zifuatwe. Lakini katika baadhi ya nchi, sheria hazitumiki kwa usawa kwa kila mtu anayeishi humo. Huko wengine wanaweza kufungwa bila sababu, wakati wengine wanaweza kuvunja sheria na hawapewi adhabu.

Hivi sivyo ilivyo Norwei au Nchi ya Norwe haipo hivyo. Kwa sababu Norwe ni nchi inayofuata sheria. Hii ina maanisha kila mtu anapaswa kufuata kanuni, na mahakama inahakikisha wanaovunja sheria wanaadhibiwa.

En lesetest om hva en rettsstat er. Teksten er oversatt med tillatelse fra zmekk.no
Mahakama inahakikisha wanaovunja sheria wanadhibiwa.

Katika nchi ambazo hazifuati sheria, watu hawafuati sheria sawa. Kwa mfano watu matajiri na watu wenye nguvu kwenye jamii, wanakwepa adhabu kwa kuwalipa polisi au hakimu.

Kama mtu ataendesha gari kupita kiwango cha mwendo kasi unaoruhusiwa na akasimamishwa na polisi anaweza walipa polisi ili asiripotiwe au asikamatwe. Hii inaitwa kutoa rushwa. Ama mtu anamjua hakimu katika kesi hivyo anapata adhabu ndogo.

Dereva anajaribu kumpa rushwa polisi

Katika nchi ambayo haifuati sheria polisi wanaweza kumfunga mtu gerezani, bila ya kuwa amaevunja sheria. Inaweza kuwa mtu huyo ana mawazo tofauti ya kisiasa ama kidini na watu wenye nguvu katika nchi hiyo.

kufungwa jela au gerezani bila ya sababu

Nchi ya Norwe haipo hivyo. Hapa kila mtu anapata hukumu ya haki akituhumiwa kuvunja sheria, na polisi wanahakikisha sheria inatumika kwa usawa kwa kila mtu bila kujali ana pesa au nguvu ya madaraka kiasi gani.

Kama waziri mkuu wa Norwei ataendesha gari kupita kiwango cha kasi, atapewa adhabu sawa kama watu wengine. Hivyo ndivyo inavyokua kuishi katika nchi inayofuata sheria.

Sheria ni sawa kwa kila mtu.


Zoezi au kazi

  1. Kwa nini inaweza kuwa sio salama kuishi katika nchi ambayo viongozi na polisi wanaweza kumfunga na kumuadhibu mtu yoyote?
  2. Katika nchi unayotoka mahusiano kati ya watu/raia na polisi yapo vipi?

Orodha ya maneno

Nchi inayofuata sheria -Nchi ambayo sheria zipo sawa kwa kila mtu

Kesi– Malalamiko ya kutokukubaliana ambapo yataamuliwa na hakimu ndani ya mahakama

Utawala wa nguvu – Uongozi wa kimabavu wa watu wachache ndio wanaoweza kufanya maamuzi ndani ya Nchi mfano viongozi wa serikalini na polisi wanaweza kumfunga na kumuadhibu mtu yoyote wanayetaka.

Rushwa– malipo ya pesa au kitu yasiyo halali yanayotolewa kwa mtu mwenye madaraka kwa siri ili aweze kumsaidia mtoaji rushwa.

Tekst og bilder er oversatt og publisert etter avtale med Zmekk.no