Fornybare energikilder // Vyanzo vya nishati isiyoisha
Katika maisha yetu ya kila siku, tunatumia umeme ( moto) mwingi. Umeme unaupata kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya nishati (nguvu). Kuna aina mbili ya vyanzo vya nishati : vyanzo vya nishati visivyoisha na vyanzo vya nishati vinavyoisha. Katika maandishi haya tutazungumzia vyanzo vya nishati visivyoisha.
Tunaposema chanzo cha nishati isiyoisha, tunamaanisha tunaweza kuitumia nishati hii bila ya kuimaliza. Nishati mpya inatengenezwa kila siku kupitia mzunguko wa asili unaojiongoza wenyewe. Mfano wa chanzo hiki cha nishati ni nishati itokanayo na maji, nishati itokanayo na upepo na nishati itokanayo na jua. Vyanzo vyote hivi utokea katika jua. Jua linavipatia vyanzo hivi nishati kwa njia tofauti.
Nishati itokanayo na maji
Nishati ya maji ni nishati inayotokano na maji yanayotiririka. Nchini Norwe, tuna maji mengi yanayotiririka katika maporomoko ya maji na mito, na tunaweza kutumia maji haya kuzalisha nishati. Jua ndio linalosababisha maji ya dunia yaweze kutembea (kutikisika). Jua hupatia joto maji mpaka kupelekea kutoa mvuke. Kisha maji hujikusanya kwenye mawingu, ambayo baadae hunyesha tena duniani. Duniani maji hutiririka kwenye mito, maporomoko ya maji na kuelekea baharini.
Nishati itakonayo na upepo
Jua hupasha joto hewa na kusababisha itembee. Kutembea huko kwa hewa tunaita upepo. Upepo ni hewa inayotembea, na tunaitumia kutengenezea nishati (nguvu). Tunaweza kutumia nishati hii kwa kuweka kata upepo (kwa kinorwei vindmøller). Kata upepo (kwa kinorwei vindmøller) sio uvumbuzi mpya umekuwa ukitumika kwa muda mrefu sana, katika kusaga nafaka (mbegu) na kutengeneza unga.
Nishati itokanayo na jua
Nishati itokanayo na jua inaweza kutumika kuyapatia joto maji na nyumba tunazoishi. Nishati itokanayo na jua inaweza kutumika pia kutengeneza umeme kwa kutumia kile kinachoitwa seli za jua (kwa kinorwey inaitwa solceller).