Fornybare energikilder // Vyanzo vya nishati isiyoisha

Denne teksten om fornybare energikilder finnes på flere språk. Tanken er at teksten skal være et supplement til andre læremidler og andre aktiviteter i opplæringen. Det er altså ikke meningen at disse ressursene skal stå alene, men at de kan brukes i innledning til arbeid med temaet.

Teksten kan, for eksempel, brukes sammen med tospråklig lærer for å aktivere elevenes kunnskaper om temaet, og å bidra til at eleven lærer fagspråk.

Scroll nedover for å finne flere ressurser.

Katika maisha yetu ya kila siku, tunatumia umeme ( moto) mwingi. Umeme unaupata kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya nishati (nguvu). Kuna aina mbili ya vyanzo vya nishati : vyanzo vya nishati visivyoisha na vyanzo vya nishati vinavyoisha. Katika maandishi haya tutazungumzia vyanzo vya nishati visivyoisha.

Bilde av lyspærer som lyser.
Bilde: Adobe Stock
Bilde av en ledning. I bakgrunnen er det en bil.
Bilde: Adobe Stock

Tunaposema chanzo cha nishati isiyoisha, tunamaanisha tunaweza kuitumia nishati  hii bila ya kuimaliza. Nishati mpya inatengenezwa kila siku kupitia mzunguko wa asili unaojiongoza wenyewe. Mfano wa chanzo hiki cha nishati ni nishati itokanayo na maji, nishati itokanayo na upepo na nishati itokanayo na jua. Vyanzo vyote hivi utokea katika  jua. Jua linavipatia vyanzo hivi nishati kwa njia tofauti.

Bilde av noe lyst på en himmel.
Bilde: Adobe Stock

Nishati itokanayo na maji

Nishati  ya maji ni nishati inayotokano na maji yanayotiririka. Nchini Norwe, tuna maji mengi yanayotiririka katika maporomoko ya maji na mito, na tunaweza kutumia maji haya kuzalisha nishati. Jua ndio linalosababisha maji ya dunia yaweze kutembea (kutikisika). Jua hupatia joto maji mpaka kupelekea kutoa mvuke. Kisha maji hujikusanya kwenye mawingu, ambayo baadae hunyesha tena duniani. Duniani maji hutiririka kwenye mito, maporomoko ya maji na kuelekea baharini.

Foto: Adobe Stock

Nishati itakonayo na upepo

Jua hupasha joto hewa na kusababisha itembee. Kutembea huko kwa hewa tunaita upepo.  Upepo ni hewa inayotembea, na tunaitumia kutengenezea nishati (nguvu). Tunaweza kutumia nishati hii kwa kuweka kata upepo (kwa kinorwei vindmøller). Kata upepo (kwa kinorwei vindmøller) sio uvumbuzi mpya umekuwa ukitumika kwa muda mrefu sana, katika kusaga nafaka (mbegu) na kutengeneza unga.

Bilde av flere vindmøller. I bakgrunnen ser man skog og fjell.
Bilde: Adobe Stock

Nishati itokanayo na jua

Nishati itokanayo na jua inaweza kutumika kuyapatia  joto maji na nyumba tunazoishi. Nishati itokanayo na jua inaweza kutumika pia kutengeneza umeme kwa kutumia kile kinachoitwa seli za jua (kwa kinorwey inaitwa solceller).

Bilde av solcellepanel som står på skrå på et gress.
Bilde: Adobe Stock
Bilde av solcellepanel på et hustak.
Bilde: Adobe Stock