Økosystem // Mfumo wa ikolojia

Denne teksten om økosystem finnes på flere språk. Tanken er at teksten skal være et supplement til andre læremidler og andre aktiviteter i opplæringen. Det er altså ikke meningen at disse ressursene skal stå alene, men at de kan brukes i innledning til arbeid med temaet.

Teksten kan, for eksempel, brukes sammen med tospråklig lærer for å aktivere elevenes kunnskaper om temaet, og å bidra til at eleven lærer fagspråk.

Scroll nedover for å finne flere ressurser


Mpangilio au mfumo  wa kiikolojia ni muingiliano au ushirikiano kati ya viumbe hai na mazingira wanayoishi. Kuna aina  nyingi tofauti za mifumo ya kiikolojia duniani. Ukubwa katika mifumo ya kiikolojia inatofautiana. Baadhi ya mifumo ya kiikolojia ni midogo, mfano bwawa la maji. Mifumo mingine ya kiikolojia ni mikubwa, kwa mfano myr (kwa kinorway) ni nyasi fupi zilizoota kwenye udongo wenye majimaji, jangwa (eneo kubwa lenye mchanga mwingi), ziwa, bahari na msitu.

Matokeo au zao la vitu visivyo na uhai (vitu visivyoishi)

Vitu ambavyo haviishi (havina uhai) katika mfumo wa kiikolojia tunaviita zao la abiotic (vitu visivyo na uhai). Mifano ya abiotic (vitu visivyo na uhai) ni hali ya hewa, udongo, mwangaza (mwanga wa jua), vitu vyenye chumvi na vitu vingine vya kikemikali ndani ya mazingira (maeneo au sehemu inayo tuzunguka).

Matokeo ya vitu vinavyoishi (vyenye uhai)

Ni vitu vyenye uhai ambavyo vinaishi kwenye mazingira (maeneo au sehemu) asilia, ambavyo tunaviita ni  zao la biotic (viumbe hai). Mifano ya mazao ya biotic (vitu vyenye uhai) ni wanyama, mimea, wadudu, bakteria na virusi. Haya ni matokeo yanayotegemea katika sababu za vitu vyenye uhai na vitu visivyo na uhai.

Viumbe hai vinategemeana

Katika mfumo wa kiikolojia viumbe hai vinavyoishi vinategemeana kwa sababu za abiotic na wanategemeana wao wenyewe katika kuishi na kuzaliana. Mimea wanategemea fangasi (sopp kwa kinorway) na wadudu viharibisha viumbe au masalia yaliyobaki katika viumbe vilivyokufa ili viweze kuwa tena udongo. Mimea inahitaji virutubisho au chakula kutoka katika udongo ili iweze kukua. Wanyama wengine lazima wale mimea ili waweze kuishi. Wanyama wengine wanategemea kupata virutubisho au chakula kwa kula wanyama wengine. Fangasi (kinorway sopp) na wadudu vinahitaji kupata chakula kutoka masalia ya mimea na wanyama walio kufa. 

Wazalishaji

Viumbe wengine wanaweza kuzalisha  vifaa vya kikaboni (nyenzo)  au vifaa visivyo vya kikaboni kwa kinorway (oganisk na uorganisk). Hizi tunaziita uzalishaji. Wazalishaji pia wanatengeneza virutubisho au chakula, na unafanyika kupitia kitendo kiitwacho  usanisinuru   (kwa kinorway fotosyntesen). Mimea na mwani za kijani zinazoota juu ya maji ( algae) ni wazalishaji katika mfumo wa kiikolojia. Wazalishaji wao wenyewe wanatengeneza virutubisho au chakula kile wanachohitaji.

Kløvereng
Mimea ya kijani ni wazalishaji.

Watumiaji

Wanyama hawawezi kujitengenezea chakula chao wenyewe. Wanategemea kula mimea au wanyama wengine. Neno lingine linalotumika badala ya kula ni watumiaji. Ndio maana tunawaita watumiaji. Watumiaji  inamaanisha sawasawa na kutumia. Ndio maana tunawaita wanyama ni watumiaji. 

En snegle spiser et blad
Konokono ni watumiaji.

Waharibifu

Waharibifu ni viumbe wanaoishi kwa kula wanyama na mimea iliyokufa. Bakteria na uyoga ni mifano ya uharibifu. Uharibifu wa kubadilisha ni muhimu katika mfumo au sababu  za ikolojia, kwa sababu upoteza na ubadilisha wanyama na mimea iliyokufa na kuwa udongo tena. Katika mchakato huu, virutubisho hutolewa kutoka kwa viumbe vilivyo kufa. Kitendo hiki kinaupatia udongo virutubisho vitakavyochukuliwa na mimea mipya. 

Bilde av en sopp i skogen
Uyoga ni kitendo cha upotezaji na ubadirishaji.

Alle bilder er hentet fra AdobeStock