Rettstaten // Nchi inayofuata sheria
Nchi zote zina sheria na kanuni ambazo lazima zifuatwe. Lakini katika baadhi ya nchi, sheria hazitumiki kwa usawa kwa kila mtu anayeishi humo. Huko wengine wanaweza kufungwa bila sababu, wakati wengine wanaweza kuvunja sheria na hawapewi adhabu.
Hivi sivyo ilivyo Norwei au Nchi ya Norwe haipo hivyo. Kwa sababu Norwe ni nchi inayofuata sheria. Hii ina maanisha kila mtu anapaswa kufuata kanuni, na mahakama inahakikisha wanaovunja sheria wanaadhibiwa.
Katika nchi ambazo hazifuati sheria, watu hawafuati sheria sawa. Kwa mfano watu matajiri na watu wenye nguvu kwenye jamii, wanakwepa adhabu kwa kuwalipa polisi au hakimu.
Kama mtu ataendesha gari kupita kiwango cha mwendo kasi unaoruhusiwa na akasimamishwa na polisi anaweza walipa polisi ili asiripotiwe au asikamatwe. Hii inaitwa kutoa rushwa. Ama mtu anamjua hakimu katika kesi hivyo anapata adhabu ndogo.
Katika nchi ambayo haifuati sheria polisi wanaweza kumfunga mtu gerezani, bila ya kuwa amaevunja sheria. Inaweza kuwa mtu huyo ana mawazo tofauti ya kisiasa ama kidini na watu wenye nguvu katika nchi hiyo.
Nchi ya Norwe haipo hivyo. Hapa kila mtu anapata hukumu ya haki akituhumiwa kuvunja sheria, na polisi wanahakikisha sheria inatumika kwa usawa kwa kila mtu bila kujali ana pesa au nguvu ya madaraka kiasi gani.
Kama waziri mkuu wa Norwei ataendesha gari kupita kiwango cha kasi, atapewa adhabu sawa kama watu wengine. Hivyo ndivyo inavyokua kuishi katika nchi inayofuata sheria.
Zoezi au kazi
- Kwa nini inaweza kuwa sio salama kuishi katika nchi ambayo viongozi na polisi wanaweza kumfunga na kumuadhibu mtu yoyote?
- Katika nchi unayotoka mahusiano kati ya watu/raia na polisi yapo vipi?
Orodha ya maneno
Nchi inayofuata sheria -Nchi ambayo sheria zipo sawa kwa kila mtu
Kesi– Malalamiko ya kutokukubaliana ambapo yataamuliwa na hakimu ndani ya mahakama
Utawala wa nguvu – Uongozi wa kimabavu wa watu wachache ndio wanaoweza kufanya maamuzi ndani ya Nchi mfano viongozi wa serikalini na polisi wanaweza kumfunga na kumuadhibu mtu yoyote wanayetaka.
Rushwa– malipo ya pesa au kitu yasiyo halali yanayotolewa kwa mtu mwenye madaraka kwa siri ili aweze kumsaidia mtoaji rushwa.
Tekst og bilder er oversatt og publisert etter avtale med Zmekk.no