Svømming i skolen// Kuogelea shuleni
Katika somo la mazoezi ya viungo vya mwili, wanafunzi watafundishwa kuogelea wakiwa ndani na nje. Kupitia shughuli mbalimbali, wanafunzi watajifunza jinsi ya kuwa salama ndani, pembeni au karibu na maji.

Mafunzo hufanyika ndani kwenye bwawa la kuogelea. Wavulana na wasichana wana mafunzo pamoja, lakini wavulana na wasichana wanabadilisha nguo za kuogelea katika vyumba tofauti vya kubadilishia nguo. Katika vyumba vya kubadilishia nguo, unavua nguo na kuoga kabla ya kuvaa nguo za kuogelea. Wanafunzi lazima waje na sabuni, taulo na nguo za kuogelea (suti ya kuogelea/bikini/suruali ya kuogelea/kaptura ya kuogelea).

Mafunzo hufanyika nje katika maji ya chumvi au maji safi. Wavulana na wasichana wanafanya mazoezi pamoja, lakini wanabadilisha mavazi ya kuogelea sehemu tofauti. Nguo za kuogelea zinategemea ni kipindi gani cha mwaka mazoezi yanafanyika (majira ama msimu wa mwaka).

Wakati wa mafunzo, wanafunzi wanapata ujuzi katika kuogelea, kuzuia na jinsi ya kufanya wanapokuwa karibu, pembeni, na ndani ya maji. Huu ni ujuzi muhimu wa kuwa nao unapokuwa unaogelea na marafiki wakati wa mapumziko.

Kama mzazi/mlezi, wewe ni muhimu kwa mafunzo (masomo) ya mtoto wako. Tafadhali wasiliana na shule ikiwa una maswali yoyote kuhusu mafunzo.

Kwa habari au taarifa zaidi kuhusu mafunzo ya kuogelea, angalia svømmedyktig.no
Imeandaliwa na Nasjonalt senter for mat, helse og fysisk aktivitet katika ushirikiano na Nasjonalt senter for flerkulturell opplæring. Vielelezo vya michoro na Thomas Madsen.