Demokrati og diktatur // Demokrasia na udikteta

Denne teksten finnes på flere språk. Tanken er at teksten skal være et supplement til andre læremidler og andre aktiviteter i opplæringen. Det er altså ikke meningen at disse ressursene skal stå alene, men at de kan brukes i innledning til arbeid med temaet.

Teksten kan, for eksempel, brukes sammen med tospråklig lærer for å aktivere elevenes kunnskaper om temaet, og å bidra til at eleven lærer fagspråk.

Demokrasia – Kuamua kwa pamoja

Demokrasia kwa jina lingine inaitwa maamuzi yatokanayo na watu wote kwa pamoja. Ni mfumo wa uongozi ambao kila mtu ana nafasi ya kutoa maoni na kushiriki katika kufanya maamuzi. Watu wanapata nafasi ya kufanya maamuzi kupitia kupiga kura kwenye uchaguzi. Demokrasia inatofautiana na mifumo mingine ya uongozi kama udikteta ambayo ni mtu mmoja anaamua. Mfumo wa uongozi nchini Norwe ni wa kidemokrasia. Hii inamaanisha kila mtu anaeishi Norwe anaruhusiwa kushiriki na kuamua jinsi jamii inavyopaswa kuwa. Watoto na vijana wanapaswa kueleza maoni yao na kusikilizwa kwa masuala yanayowahusu.

Demokrasia ni neno lenye mchanganyiko wa maneno mawili ya Kigiriki “demos” inayomaanisha watu na “kratein” inayomaanisha mtawala ama utawala. Wazo la demokrasia liliibuka mji wa Athens karibia miaka 2500 iliyopita. Nchini Norwe kuna vyama mbalimbali vya siasa ambavyo vina maoni tofauti juu ya jinsi gani jamii inapaswa kuwa. Wakati kuna uchaguzi wa wabunge, watu wazima wenye miaka 18 na zaidi wanaweza kupiga kura kuchagua chama wanacho kubaliana nacho zaidi.

Tegning av mange mennesker som står i kø for å stemme ved valg

Uhuru wa kujieleza

Katika demokrasia kuna uhuru wa kusema. Hiyo ni kwamba kila mtu anaweza kusema na kuandika anachomanisha, bila kuadhibiwa kwa hilo. Kuanzia umri mdogo tunajifunza kutoa mawazo, hisia na maoni yetu. Wakati huo huo ni muhimu kuheshimu na  kujifunza watu wengine wanaweza kuwa na mawazo tofauti na yale tuliyonayo. Unapozidi kukua, maoni yako yanazidi kuzingatiwa.

Demokrasia – vyombo huru vya habari

Katika demokrasia vyombo vya habari hutumika kutoa maoni tofauti tofauti. Vyama vya siasa Norwe vinatumia vyombo vya habari tofauti kufikia watu haswa kabla ya uchaguzi. Tunaweza kufuatilia kwenye runinga(TV), magazeti, redio na kwenye mtandao (intaneti) wakati wanasiasa wanajadili sera zao jinsi masuala ya kijamii yanavyotakiwa kuwa.

Terning av mange mennesker som intervuer en person. Alle journalistene har mikrofoner
Illustrasjon: Adobe Stock MicroOne

Udikteta – wachache huamua

Baadhi ya nchi zina mfumo wa uongozi unaoitwa udikteta. Uongozi wa udikteta ni wa mabavu, unao lazimisha maamuzi ya mtu mmoja ama watu wachache ambao wanamua jinsi ya kuongoza nchi. Hairuhusiwi kutoku kubaliana na watu wanaoongoza nchi. Watu wanaosema ama kuandika kitu ambacho serikali (mamlaka) haipendi wanaweza kuteswa na kufungwa gerezani. Wengine wanauawa kwa sababu ya kutoa maoni yao.

Ni kawaida kutaja aina tofauti za udikteta kulingana na watu wanaotawala ni wangapi (au ni nani) na jinsi gani ukosefu wa uhuru ulivyo:

  • Ikiwa nguvu ipo kwa mtu mmoja, hapo inamaanisha udikteta wa mtu mmoja mfano Adolf Hitler wa Ujerumani, Josef Stalin wa iliyokuwa umoja wa Soviet, Francisco Franco wa Uhispania.
  • Ikiwa nguvu ipo kwa watu kadhaa, hapo ina maanisha udikteta wa ujamaa (urafiki) ama uongozi wa watu wachache, kama ilivyo katika mataifa mengi ya kijeshi na nchi zinazoongozwa na chama kimoja.

Udikteta – sauti moja tu inapaswa kusikika

Katika nchi zenye udikteta serikali (mamlaka) zinamiliki ama kudhibiti vyombo vya habari. Magazeti, redio na runinga (TV) zinaeleza habari zile ambazo serikali (mamlaka) inataka watu wasikie. Hairuhusiwi kusema ama kuandika kile unachomanisha. Serikali (mamlaka) inadhibiti kile watu wanasema ama kuandika.

Det er mulig å skrive ut eller bruke innhold fra dette innlegget på flere måter.

Legg merke til at innhold kan være ulikt lisensiert.

Regler for bruk av teksten 

Denne teksten har lisensen CC BY-NC 4.0. Denne lisensen gir deg rett til å dele og bruke dette innholdet på visse vilkår:

  • Du må alltid oppgi hvem som har laget innholdet.
  • Du kan bare dele innholdet med samme lisens som det opprinnelige innholdet.
  • Du kan ikke benytte materialet til kommersielle formål.

Regler for bruk av bilder i teksten

Bildene i denne teksten kan ha ulike linsenser. Les mer om hvert bilde.

  1. Tegning av mange mennesker som står i kø for å stemme ved valgAdobeStock_707298019-1024x461.jpeg — Illustrasjon: oksaoksaoksa stock.adobe.com

  2. Journalistikk.jpg

Regler for bruk av lydfiler i innlegget

Denne teksten har lisensen CC BY-NC 4.0. Denne lisensen gir deg rett til å dele og bruke dette innholdet på visse vilkår:

  • Du må alltid oppgi hvem som har laget innholdet.
  • Du kan bare dele innholdet med samme lisens som det opprinnelige innholdet.
  • Du kan ikke benytte materialet til kommersielle formål.