Dom og straff // Hukumu na adhabu
Asubuhi moja Erik anagundua kuwa mtu fulani ameiba gari lake. Anapata taarifa au kidokezo kwamba Jonas ndiye mwizi.
Mtu anapovunja sheria, ni kazi ya polisi kufanya utafiti wa kuchunguza kesi hiyo. Hivyo ina maana wanajaribu kujua nini kilitokea. Wanaongea au wanazungumza na watu ambao wameona au kusikia kitu, na kuchunguza eneo la tukio la uhalifu ulipofanyika au kutokea. Eneo la tukio la uhalifu ni sehemu au mahali ambapo kitendo cha uhalifu kilifanyika.
Polisi wanaamini wanaweza kuthibitisha kuwa Jonas ameiba gari hilo. Kwa hivyo, kesi itafanyika, ambapo itaamuliwa ikiwa hii ni sahihi. Kesi itafanyika katika mahakama. Kuna aina nyingi za mahakama nchini Norway. Mahakama ya chini kabisa inaitwa Mahakama ya Wilaya. Hapa, mwendesha mashtaka, ambaye ni mwakilishi wa polisi katika kesi hiyo, atajaribu kuthibitisha kwamba Jonas ana hatia (amefanya makosa). Jonas ana wakili wake ambaye atamtetea katika kesi hiyo. Mwendesha mashtaka na upande wa utetezi wana mashahidi kwa pamoja, ambao wao ndio watakaowasaidia kujua kilichotokea.
Ni mahakimu (waamuzi au majaji) wanao amua kama Jonas amefanya kosa (hatia) au la, na ni adhabu gani anapaswa kupewa. Mahakimu (waamuzi au majaji) ni wataalamu wa sheria na kanuni.
Iwapo Jonas na mtetezi wake hawataridhika na matokeo, wanaweza kukata rufaa ya kesi hiyo kutoka Mahakama ya Wilaya hadi Mahakama ya rufani. Mwendesha mashtaka anaweza kufanya hivyo pia. Hivyo kesi itakuwa ni mpya (itasikilizwa upya). Katika Mahakama ya rufaa, pamoja na majaji, kuna jopo la majaji. Hawa ni watu wa kawaida ambao husaidia kuamua kama mshtakiwa ana hatia (amefanya kosa) na ni adhabu (hukumu) ya muda gani anapaswa mtu kupewa.
Kuna mahakama nyingine nchini Norway inayoitwa Mahakama ya juu. Kuna moja tu, na hapa mtu anaweza kukata rufaa kwa kesi maalumu tu. Kwa mfano, ikiwa unaamini kuwa katiba au haki za binadamu zimekiukwa (zimevunjwa).
Kuna aina mbalimbali za adhabu kwa kuvunja sheria. Kwa makosa madogo, ni kawaida kulipa faini. Kisha unalipa pesa kwa serikali kama adhabu. Unaweza pia kuhukumiwa kufanya kazi bure kwa jamii kwa muda. Inaitwa huduma kwa jamii. Makosa makubwa zaidi yanaadhibiwa kwa kifungo cha kwenda jela (gerezani).
Hakuna hukumu ya kifo au kifungo cha maisha nchini Norway. Hukumu kali zaidi unayoweza kupata nchini Norway ni kifungo cha miaka 21. Lakini wafungwa wengine ni hatari sana kuachiliwa tena katika jamii baada ya miaka 21. Hivyo wanaweza kuhukumiwa waendelee kuwa kizuizini (gerezani), na hawataachiliwa hadi iwe salama kwa jamii.
Watoto chini ya miaka 15 hawawezi kupata kifungo cha gerezani nchini Norway.
Ordliste
Uchunguzi au kufatilia Chunguza kilichotokea |
Eneo la tukio la uhalifu Ni kitu kisicho halali (haramu) kilipotokea au uhalifu ulipofanyika. |
Hakimu au Jaji Wale wanaoamua kama sheria imevunjwa katika kesi mahakamani |
Rufaa Omba kuhusu kupata kusikilizwa kwa kesi upya. |
ni jopo (kikundi) la majaji wanaotoa maamuzi kwa kesi inayoendelea, jaji au hakimu hawezi kumtia mtu hatiani bila kusikia walichoamua. |
Tekst og bilde er gjengitt og oversatt med tiltatelse fra Bergen kommune og zmekk.no