Mesopotamia // Mesopotamia
Mito Eufrat na Tigris iko ndani ya nchi ya Uturuki, Irak na Syria. Kwa miaka 6000 iliyopita, eneo kubwa la maeneo yaliyopo katika nchi hizo zilikuwa zinaitwa Mesopotamia, ambayo inamaanisha “nchi katikati ya mito”.
Hali ya hewa katika eneo, ilikuwa ni joto wakati wote na ni nzuri, lakini pia palikuwa pakavu sana. Hata hivyo, matunda mengi yanayouzwa nchini Norway yanatoka eneo hilo. Eneo hilo lina rutuba (udongo mzuri kwa kilimo). Inakuwaje ni pakavu sana na wakati huo huo kuna rutuba?
Kama ulivyoweza kukisia (kubahatisha), mito ndio sababu ya maelezo. Bila mito mikubwa, eneo hilo lingekuwa jangwa zaidi, na hata hivyo hakuna kitu karibu kingeweza kukua na kumea (kustawi) huko.
Katika msimu wa mvua nyingi au masika, wakati theluji au barafu kwenye milima inayeyuka, mito ina furika. Maji yana panda na kufurika juu ya kingo sake za upana. Wakati maji yame pungua na mito inaporudi kawaida katika kingo zake za upana, huacha matope yenye rutuba kwenye udongo. Matope hayo yanakuwa na udongo mzuri na wenye virutubisho.
Watu katika Mesopotamia walitengeneza mbinu na vifaa au zana nyingi nzuri za kutumia maji kwa njia bora zaidi. Kwa maji yote waliyokuwa nayo, wangeweza kufanya udongo kuwa na rutuba na kulima kilimo chochote karibu na walichotaka. Pia kwa kuongezea, kulikuwa na samaki wengi katika mito.
Wakulima wa kwanza
Watu waliokuwa wanaishi Mesopotamia walikuwa wakulima wa kwanza. Walikuwa wa kwanza kuanza kulima ngano. Kwa kuandaa shamba, kumwagilia na mbolea udongo waligundua kwamba udongo unakuwa na rutuba nyingi. Hii iliwawezesha kuvuna nafaka za ngano mara kadhaa katika kipindi cha mwaka. Mazao makubwa na chakula zaidi kiliwafanya kwamba waweze kukusanya na kuhifadhi chakula kwa matumizi ya baadaye. Kwa kuwasaidia katika kazi zao, walitumia wanyama kama vile ng’ombe na farasi. Watu wa Mesopotamia walikuwa wa kwanza kufuga wanyama wa nyumbani.
Kulikuwa na vitu vingi vya kuishi katika Mesopotamia, hiyo ilipelekea watu wengi kuhamia huko. Na hivyo ndivyo ikatokea mji wa kwanza duniani. Hii ilikuwa kwa miaka mingi ya elfu iliyopita. baada ya muda mji ulikuwa umepangiliwa vizuri. Walikuwa na shule na jeshi. Mesopotamia inajulikana kwa hekalu zake, zilizokuwa zinaitwa ziggurat na majengo mengine mazuri. Watu walikuwa na taaluma/kazi mbalimbali. Watu wengine wanawaita watu wa Mesopotamia kuwa watu wa kwanza wa kitamaduni.
Uvumbuzi
Upande wa kusini mwa Mesopotomia kuna nchi iitwayo Sumer. Wasummeri walivumbua vitu vingi vya muhimu pamoja na hisabati na jiometri. walitengeneza mfumo wa namba ukiwa na 60 kama namba ya msingi. Tunatumia baadhi ya hivyo leo hii. Saa moja ina dakika 60 na dakika moja ina sekunde 60. Duara tunaligawa kwenye nyuzi za digrii 360.
Mfumo wa namba wenye 60 kama namba za msingi
Kati ya miaka 3500 na 3000 kabla ya Kristu waliendeleza mfumo wa kuandika ulioitwa mwandiko wa kikabari (kileskrift). Kwanza ilikuwa mwandiko wa kikabari (Kileskrift) ni maandishi ya picha. baada ya muda ikafupishwa/rahisishwa, na picha zikabadilishwa na kuwa alama. Wasumeri waliandika kwenye ubao wa udongo na kwenye mawe. sanaa ya kuandika ikasambaa mashariki ya juu na magharibi ya juu pamoja na Misri. Uvumbuzi mwingine kwa mfano ni gurudumu (pinee) na kifaa cha kulimia plau pezi (jembe la kulimia la wanyama). Isitoshe waliweka mkuku kwenye boti zao ili zisipinduke kwa urahisi na wakaanza kutumia tanga (kitambaa kikubwa kinachofungwa kwenye boti) ili wasilazimike kupiga kasia muda wote.
Miji
Wasumeri walijenga miji mizuri. Mji mkubwa katika Sumeri unaitwa Uruk. Mji Ur ulikuwa mji muhimu wa biashara, uliounganishwa na bahari. Kila mji ulikuwa taifa la kujitegemea lenye mfalme wake. Wafalme walikuwa na nguvu nyingi, pia walikuwa viongozi wa kidini. Katika miji aliishi mfalme, watumishi wake, wachungaji/ makuhani na mafundi.
Mara nyingi kulikuwa na ukuta kuzunguka mji wote kwajili ya kuulinda dhidi ya maadui. Wakulima waliokuwa wanaishi katika eneo la kuzunguka mji, ilibidi walipe kodi kwa mfalme kama vile ngano, nyama, samaki na mboga za majani. Wasumeri hawakutumia pesa, ilikupata vitu au bidhaa. Walibadilishana vitu walivyokuwa wanahitaji. Wafanyabiashara walisafiri nje ya nchi na kubadilishana kwa shaba na dhahabu. Mafundi walibadilishana vyakula kwa vitu au bidhaa kama vyombo vya udongo, vito (vitu vya thamani vya urembo na mapambo) na nguo na vifaa mbalimbali vya nyumbani.
Maneno muhimu kwenye andiko
Kupangilia
.inamaanisha kuweka kitu ili kiweze kuunda kitu kamili.
kukusanya
inamaanisha kuweka pamoja.
kuhifadhi
inamaanisha kuweka kwa ajili ya kutumia baadae.
kufupisha
.inamaanisha kufanya kitu kuwa rahisi kwa kifupi.
kutokea
inamaanisha kitu kinakuwa, kinaanza ama kinakuja.
utumiaji wa faida
inamaanisha kufaidika na kitu kwa uzalishaji au faida, kutumia kitu kikupe kitu.
kulima
inamaanisha kuzalisha kitu kwa mfano mimea.
kubadilisha
inamaanisha kumpatia mtu kitu au kutoa kitu na kupata kitu kingine.
kuvuna
inamaanisha kuchukua mazao yaliyokomaa, yale ambayo umeyalima.
kufurika
inamaanisha maji yaliyofurika au yaliyojaa zaidi (mafuriko).
kuongezeka au kupanda / kupungua au kuzama
kupanda inamaanisha kitu kimeongezeka au kimekwenda juu. kuzama inamaanisha kitu kimepungua ama kimekwenda chini.
kuweka mbolea
inamaanisha kuweka kwenye udongo vitu vyenye virutubisho kama kinyesi cha wanyama ili mimea iweze kukua vizuri.
Ilustrasjon1: Karl Musser, translated labels by User:Mathias-S, CC BY-SA 2.5, via Wikimedia Commons