Valg og politiske partier // Uchaguzi na vyama vya kisiasa
Nora ametimiza au amefikisha umri wa miaka 18 na anaweza kupiga kura katika uchaguzi. Hana uhakika ni chama gani kinamfaa yeye zaidi.


Kuna vyama vingi tofauti vya kisiasa. Ili kujua ni chama gani Nora kitamfaa na kukipigia kura, Nora anasoma mipango (ilani) ya vyama vya kisiasa. Mipango au ilani za chama ni malengo au maelezo ya vyama kwa kifupi ambayo wanasiasa huandika ili kuonyesha kile wanachofikiria, na kile wanachotaka kufanya ili kufikia malengo yao ya kuchaguliwa katika uchaguzi . Vilevile, Nora hufuatilia kwa kusoma magazeti na kuangalia TV au runinga kabla ya uchaguzi. Kule, viongozi wa vyama mbalimbali vya kisiasa hukutana katika mazungumzo ya majadiliano ambapo hujadili masuala muhimu ya kisiasa kutoka katika vyama tofauti. Kila chama kinajaribu kuwashawishi watu wote au jamii kwamba wanapaswa kukipigia kura ama kukichagua chama hicho.
Kuna uchaguzi kila baada ya miaka miwili nchini Norwe, na kuna aina mbili tofauti za uchaguzi. Kuna kuwa na uchaguzi mkuu wa bunge na kuna kuwa na uchaguzi wa manispaa (serikali za mitaa). Raia wote wa Norwe walio na umri wa miaka kuanzia 18 na zaidi wanaweza kupiga kura katika uchaguzi wa bunge, na katika uchaguzi wa manispaa (serikali za mitaa), mtu yeyote aliyefikisha umri wa miaka 18 na zaidi, ambaye ameishi Norwe kwa angalau miaka 3 anaweza kupiga kura.

Katika uchaguzi wa bunge au wabunge, unapigia kura na kuchagua chama kipi ambacho kitapata wawakilishi wengi katika bunge. Vyama vinavyopata kura nyingi huunda serikali na kukubaliana kuhusu kuchagua au kuteua waziri mkuu kutoka katika chama kilichoshinda kwa kupata kura nyingi. Bunge na serikali huamua juu ya mambo muhimu yanayohusu nchi nzima.
Mojawapo ya maswala muhimu zaidi kwa Nora ni kwamba, njia nyingi za baisikeli zinapaswa kujengwa katika eneo lake la karibu. Mambo ya ngazi ya sehemu hiyo haya shughulikiwi na uongozi ngazi ya bunge na serikali. Na ndio maana Norwe ina demokrasia sehemu ya ngazi ya manispaa (serikali za mtaa). Wanasiasa wa sehemu za manispaa (serikali za mitaa) wana mawasiliano ya karibu na watu wanaoishi nao na wanaweza kusikiliza na kuweka sawa malengo yao kulingana na kile watu au wananchi wanahitaji.

Katika uchaguzi wa manispaa (serikali za mitaa), mabaraza ya kata na manispaa huchaguliwa. Mabaraza ya kaunti au mkoa husimamia kaunti au mkoa na kusaidia manispaa zote kushirikiana. Kaunti au mkoa pia inawajibika na miongoni mwa mambo mengine, shule za sekondari ya juu, makumbusho na huduma za afya ya meno kwa kila mtu anayeishi katika kaunti au mkoa huo.


Uongozi wa manispaa hufanya maamuzi ya kuamua katika manispaa. Vyama vinavyopata kura nyingi ndivyo vinavyopata nafasi ya uongozi katika manispaa. Kila uongozi wa manispaa unaongozwa na meya. Manispaa inawajibika pamoja na mambo mengine, shule, nyumba za wazee walio wagonjwa, usaidizi wa msaada wa kijamii, shule za chekechea na barabara au njia. Uongozi wa manispaa ndio unao amua kama ujenge njia nyingi za baisikeli au kinga, kama Nora anavyohitaji.
Nora amepata chama ambacho kinahusika zaidi na mipango ya njia za usafiri wa baisikeli au kinga na anakipigia kura katika uchaguzi wa manispaa (serikali za mitaa). Kama wakipata kura za kutosha, wanaweza kujenga njia mpya za usafiri wa baisikeli katika manispaa.

Ordliste
Partiprogram – Ilani |
Muhtasari au maelezo ya nini malengo ya chama kinamaanisha kitafanyia kazi |
Stortingsvalg – uchaguzi wa bunge |
Uchaguzi wa wakilishi wa kisiasa watakao pata nafasi kwenye bunge na kuunda serikali |
Lokalvalg – uchaguzi wa manispaa (serikali za mataa) |
Uchaguzi wa bunge la mkoa au kaunti na uongozi wa manispaa |
Fylke Kaunti au mkoa |
Eneo la kijeografia. Norwe ina kaunti au mikoa 19. |
Kommune – Manispaa |
Eneo la kijografia. Norwei ina manispaa nyingi zaidi ya mia moja |
veier- njia au barabara |
Sykkelveier – njia au barabara za kupita baiskeli au kinga |