Samene // watu wa Wasami
Idadi ya watu wa sami ni kati ya 60,000 hadi 70,000. Ndani ya nchi ya Uswidi kuna watu wasami takribani 17,000. Ndani ya Ufini au Finland wanaishi wasami takribani 7500 na ndani ya nchi ya Urusi wanaishi takribani ya wasami 2000. Lakini Ndani ya Norwei wanaishi takribani wasami 40,000. Wengi wao wanaishi kaskazini mwa mlima wa chumvi (kwa kinorwei unaitwa Saltfjellet) au ndani ya miji mikubwa, mfano mji wa Oslo.

Watu wa jamii ya wasami ni watu wanaoishi kiasili
Wasami ni watu wanaoishi kiasili. Hii ina maanisha watu wa jamii ya sami waliishi kaskazini mwa nchi ya Norwei, Ufini (Finland), Uswidi /Sweden na Urusi kwa muda mrefu sana. Waliishi huko hata kabla ya mipaka inayozigawa nchi haijaanzishwa.
Watu wa kiasili “wasami” mara nyingi wanakua na utamaduni wao au tamaduni zao ambazo zinatofautiana na watu wengine wote ndani ya nchi wanayoishi. Ndani ya dunia au ulimwenguni kuna jamii za watu mbalimbali wanaoishi kiasili. Kwa mfano ni wakurdi wenye asili ya Iran, Iraki, Syria na Uturuki.
Mashindano ya mbio za mnyama kulungu (reindeer)
Mbio za mnyama kulungu ni michezo maarufu kwa watu wa sami wanaomiliki wanyama aina ya Kulungu. Katika mashindano ya kukimbia, mwanariadha au mtu anayekimbia anavaa kifaa cha kuteleza kwenye barafu / theluji kwenye miguu yake na anashikilia kamba iliyofungwa kwa mnyama Kulungu. Katika mashindano mengine mwanariadha anakaa juu ya kiti cha kutelezea kwenye barafu/theluji kilichofungwa kwa uimara nyuma ya mnyama Kulungu (reindeer). Mnyama kulungu anaekimbia haraka sana hukimbia kilomita 60 kwa saa moja. Mashindano ya mbio za kulungu yana andaliwa kutafuta bingwa wa Norwei na bingwa wa Nchi za kinordic.

Siku ya kitaifa ya watu wa sami
Siku ya kitaifa ya watu wa Sami inaadhimishwa kila tarehe 6 ya mwezi wa pili. Siku hii inaadhimishwa kwa pamoja na Wasami wote ndani ya Norwei, Uswidi (Sweden), Ufini (Finland ) na Urusi. Siku inaadhimishwa kukumbuka mkutano wa kwanza wa kitaifa wa wasami uliofanyika mnamo tarehe 6 mwezi wa pili mwaka 1917 mjini Trondheim. Walikutana watu wa Sami kutoka Norwei na Uswidi kwa mara ya kwanza, kuzungumzia masuala yanayowahusu watu wa Sami.
Siku ya kitaifa ya watu wa Sami ni sikukuu rasmi ya kitaifa nchini Norwei, siku ina adhimishwa na kusherekewa kwa bendera ya Norwei na watu wa Sami. Sherehe za maadhimisho hufanyika sehemu mbalimbali nchini Norwei. Tromsø wanasherekea wiki nzima kwa shughuli mbalimbali kwa mfano matamasha na mbio za kulungu. Nyimbo ya watu wa sami ni “Sámi soga lávlla” inayo maanisha wimbo wa watu wa Sami.
Kwa kisami siku ya kitaifa tunasema (Lihku beivviin!) inayomaanisha “hongera na siku yako”.
Bendera ya watu wa Sami

Bendera imehamasishwa na watunzi wa mashairi toka kwa watu wa Sami, na kuwakilishwa kama ni watoto wa kike na kiume wa jua. Duara kwenye bendera ina maanisha jua na mwezi.
Kuna bunge la watu wa sami ambalo lina amua juu ya matumizi ya bendera. Tarehe 6 mwezi wa pili tunasema: (Lihku beivviin!) Ina maanisha “Heri ya siku ya kuzaliwa! au Hongera na siku yako!”.

Lugha ya wasami
Lugha ya wasami si lugha iliyo moja pekee, ni mjumuiko wa makundi ya lugha mbalimbali. Lugha ya sami inafanana na lugha ya kifinland, kiestonia na kihungary. Lugha ya wasami wa kaskazini ndio kundi kubwa la lugha ya watu wa Sami. Wasami kutoka Norwei, Uswidi na Ufini wanatumia lugha ya wasami wa kaskazini. Lugha ya wasami wa kusini haitumiki tena katika lugha ya kila siku katika familia nyingi. Ni afadhali kidogo na lugha ya lule sami, kwa sababu kuna watoto wengi wanao soma kwa lule sami nyumbani na shuleni.
Bures (inatamkwa Bores) ina maanisha Habari kwa lugha ya wasami wa kaskazini.
Lavvo na pulk ni maneno ya kisami tunayoyatumia kwenye lugha ya kinorwei.





