Hva skjer når kongen dør?// Nini kinatokea mfalme anapokufa?
Ijumaa ya tarehe 28 mwezi wa nane alikufa mfalme Harald. Watu wengi wanahuzunika kwa sababu ya kifo chake. Utaona bendera ikiwa nusu ya mlingoti, watu wanaoweka maua na watu wanaozungumza kuhusu mfalme kwenye tv na taarifa za habari. Oslo watu wengi wamekusanyika mbele ya jumba la mfalme kama njia ya kuonesha heshima.



Ni kitu cha kawaida kabisa kwa mfalme kufa anapokuwa mzee, hii ni kama vile watu wengine. Ikiwa inatokea, nchi ya Norwe tayari ina mipango ya nini kitakacho endelea.
Norwe inapata mfalme mpya


Mwanamfalme mteule ni mtoto wa kiume wa mfalme. Anapokufa mfalme Harald, mwanamfalme mteule Haakon anakuwa mfalme. Mfalme mpya amechagua kuitwa mfalme Haakon VIII.
Vitu vingi nchini Norwe vinaendelea kama kawaida. Watu wakubwa wenye majukumu katika nchi, wanajua nini wanatakiwa kufanya. Serikali, bunge (stortinget), polisi, shule, hospitali na wote wengine kwenye jamii wanaendelea na kazi zao.
Ni ruhusa kuhuzunika
Baada ya mfalme kufa, watu wengi watazungumza kuhusu yeye, kumfikiria, na kumkumbuka. Nafasi na sehemu mbalimbali utaona, soma ama kusikia kuhusu maisha ya mfalme Harald. Yeye ameishi kwa muda mrefu, amekuwa katika vitu vingi na amefanya vitu vingi vizuri kwa Norwe.

Karibuni kutafanyika mazishi ya mfalme Harald. Yatafanyika Oslo Domkirke. Watu wengine wanakuwa na huzuni sana pale mfalme anapokufa. Japo kuwa hawajawahi kukutana nae, wengi wanajisikia kuwa wanamjua. Hii ni kwa sababu amekuwa akionekana kunapokuwa na matukio muhimu, wakati mgumu na wakati wa vitu vizuri nchini Norwe. Watu wengi wanasema mfalme Harald alikuwa ni kama babu kwa watoto wote na vijana nchini Norwe.
Watoto pia wanaweza kuitikia kwa namna tofauti. Baadhi yao wanakuwa na huzuni au wasiwasi. Wengine wanakuwa na hamu ya kujua na wanakuwa na maswali (maulizo) mengi. Na wengine hawafikirii sana juu ya jambo hilo. Miitikio hii yote ni ya kawaida kabisa.


Upo salama
Japo kuwa unasikia watu wengi wanazungumza kuhusu mfalme amekufa, Norwe haipo katika hatari. Nchi inaendelea kufanya kazi. Unaweza kwenda shule, kuwa pamoja na marafiki, kucheza, kwenda kufanya mazoezi na kuendelea kufanya vitu unavyofanyaga kama kawaida.
Kama habari zinakufanya uwe na wasiwasi, inaweza kuwa jambo zuri kuzungumza na mtu mkubwa unaemuamini. Watu wakubwa wanaweza kukuelezea kitu unachowaza na kutaka kujua, na uhitaji kufuatilia taarifa za habari zote.
Jambo la maana zaidi la kukumbuka ni hili: Wakati mfalme anakufa, Norwe iko na mpango. Mfalme mpya anachukua nafasi yake, watu wakubwa wanaangalia jamii na maisha ya kila siku yanaendelea.











